Tuesday, 21 November 2017

UPEKEE WA MTU KATIKA UUMBAJI WA MUNGU.

BWANA Yesu KRISTO MWOKOZI PEKEE asifiwe sana!
Karibuni sana katika katika blog hii tuweze kujifunza mambo yanayohusu UFALME WA MUNGU!

SOMO : UPEKEE WA MTU KATIKA UUMBAJI WA MUNGU!

Mbingu na nchi na vyote viijazavyo vimeumbwa na MUNGU, na MUNGU ameumba kila kitu kwa JINSI YAKE  (namna yake, upekee, UNIQUENESS.)

Kila kitu MUNGU alichoumba ni CHEMA, Muhimu hapo ni kutambua KUSUDI la kila kitu alichoumba MUNGU, zaidi ya hapo vinaweza kutumiwa tofauti na Mpango wa MUNGU.

MWANZO 1:31 
MUNGU akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana.

Muhimu :UUMBAJI WA MUNGU lengo lake kubwa ni kupanua UFALME WA MUNGU toka MBINGUNI hadi Duniani, MUNGU mpango wake mkubwa ni KUYAFANYA MAPENZI YA MBINGUNI yafanyike pia duniani. (yale yaliyoko juu MBINGUNI yaonekane duniani)

MUNGU BABA MUUMBA, ILI Kufanikisha Mpango wake wa KUENEZA UFALME WAKE DUNIANI, akaamua KUMFANYA MTU ili huyu amwakilishe Duniani kwa kutunza, kulinda na kuongeza UFALME kwa njia ya UUMBAJI WA MUNGU!

NOTE THIS FIRST GOD'S PLAN FOR CREATION OF MAN.

Mwanzo 1:26 - 31.
"MUNGU akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu ;wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi "
" MUNGU akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa MUNGU alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba "

" MUNGU akawabarikia, MUNGU akawambia,ZAENI, MKAONGEZEKE, MKAIJAZE NCHI, NA KUITIISHA ; MKATAWALE SAMAKI WA BAHARINI, NA NDEGE WA ANGANI, NA KILA KIUMBE CHENYE UHAI KIENDACHO JUU YA NCHI "


🎤UPEKEE WA MTU.


  • Mtu ni kiumbe pekee ambaye MUNGU anaonyesha umuhimu mkubwa wakati wa uumbaji. 
  • Tumeumbwa kwa MFANO WA MUNGU. 
  • Tumeumbwa kwa SURA YA MUNGU. 
  • Mtu ndiye aliyepewa uwezo wa kutawala viumbe vingine :
  • MUNGU alitupa Pumzi ya Uhai kutoka kwake. 
  • Tofauti na viumbe vingine, MTU ana HISIA, AKILI, MAAMUZI (EMOTIONS, WILL, CHOICE). 
🎤VITU MUHIMU ALIVYOMBIWA MTU BAADA YA UUMBAJI. 
  1. ZAENI (BE FRUITFUL) : MUNGU amemwumba mtu na ndani ya mtu kuna vipawa, zawadi, kusudi, maono (gifts, potentials, relationships, visions and purposes).These are needed by others but many people die without being FRUITFUL!! Please there are more inside you, give them out to benefit others! 
  2. MKAONGEZEKE (MULTIPLY) : God does not need us to remain the same each day, each month, each year.. Because we are His own Image Creatures..we must seek to grow and multply all areas of Life so that we can influence and fill the Earth with HIS Glory and Kingdom... Don't stay at the same Level!
  3. MKAIJAZE NCHI(REPLINISH THE EARTH) : To fill the Earth with Kingdom of God through family, principles of GOD, Gospel. 
  4. KUITIISHA NCHI (SUBDUE)
  5. MKATAWALE VIUMBE HAI (HAVE DOMINION OVER OTHER LIVING THINGS) 
WANADAMU bado sisi ni wa muhimu kwa MUNGU, tunayo sura yake. Na MUNGU anaitafuta Sura yake ndani ya mwanadamu iliyopotea baada Ya ANGUKO la Mwanadamu wa Kwanza. 

YESU KRISTO amekuja kuturejesha katika mpango wa MUNGU wa Awali! 
LUKA 19:10 "KWA KUWA MWANA WA ADAMU ALIKUJA KUTAFUTA NA KUOKOA KILE KULICHOPOTEA 
"
MUNGU ANATUPENDA sana, mpaka aliamua kuchukua GHARAMA YA Kuja KUTUOKOA na Kuturudisha katika FURAHA YA MILELE aliyoweka tangu awali kwa wote WAMWAMINIO YESU KRISTO MWOKOZI PEKEE!

Barikiwa sana wote! Somo hili litaendelea... UTAPATA KUJUA WEWE ULIVYO WA THAMANI PALE UNAPOAMUA KURUDI KWA BABA MUNGU MUUMBA WETU!!
0753775948. Jb

Wednesday, 26 July 2017

SHARING THE GOSPEL (KWA NINI INJILI YA YESU KRISTO INAHUBIRIWA).

Hellow wana wa Mungu, ninakukaribisha katika blog hii ambayo utapata mafundisho mbalimbali kuhusu ufalame wa Mungu na maisha yako. Karibuni sana na BARAKA NA NEEMA ZITOKAZO KWA MUNGU ZIWE PAMOJA NAWE! 

SOMO: KWA NINI INJILI YA YESU KRISTO INAHUBIRIWA DUNIANI? (sharing the Good news). 

MATHAYO 28: 18-20. "Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi, na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siki zote, hata ukamilifu wa dahari.

MARKO 16:15-20.  LUKA 24:46-49,YOHANA 20:19-23, Matendo ya mitume 1:8. Ni maneno ya mwisho ya Bwana Yesu kabla ya kurudi kwa Baba Mbinguni, anaagiza Wanafunzi wake kwa Habari ya kupeleka Habari za Ufalme wa Mungu Ulimwenguni Kote. NI AMRI KWA KILA MWAMINI KATIKA IMANI YA YESU KRISTO. 

A:MAANA YA UINJILISTI ni kuzungumza, kupeleka, kumwambia mtu au watu habari njema za UFALME WA MUNGU. (good news or The Gospel of Jesus Christ).

MATHAYO 3: 2 "TUBUNI KWA MAANA UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA" Ni sauti ya Yohana Mbatizaji.

MATHAYO 4:17 "Tokea wakati huo YESU alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni ;kwa maana ufalme wa Mungu umekaribia"  Ni sauti ya Yesu Kristo. 

MATENDO YA MITUME 2: 38 "Petro akawambia, Tubuni mkbatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu"  Ni sauti ya petro.

MATENDO 17:30 "Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni ; bali sasa anawaagiza watu wote  wa kila mahali WATUBU"  Ni sauti ya paulo. 

🎤 Kiini cha Maneno yote na Biblia Ni UKOMBOZI WA MWANADAMU. Watu wanaitaji kusikia Habari za Msamaha wa dhambi ambao Mungu Baba ametoa kupitia njia ya kumwamini Yesu Kristo..

B: KWA NINI HABARI NJEMA ILIKUWA LAZIMA( why is the "Good News" necessary?

  1. MUNGU, ambaye ni mwenye Haki na Mtakatifu, alituumba KWA MFANO NA SURA YAKE (MWANZO 1:26-28). Mungu Baba kupitia Yesu Kristo anatafuta kurudisha Sura yake katika Utukufu wake.                                                                                                               LUKA 19:10 "KWA KUWA MWANA WA ADAMU ALIKUJA KUTAFUTA NA KUOKOA KILE KILICHOPOTEA"      Watu wote ni sura ya Mungu, wanahitaji kuokolewa.                       TOKA mbinguni Mungu anatazama sura yake, Hataki iendelee kuwa chini ya Utumwa wa giza na shetani. 
  2. Mwanadamu wa kwanza Adamu, alianguka katika DHAMBI na kuwa nje ya Ushirika pamoja na Mungu,  hivyo akaipoteza SURA YA MUNGU aliyoumbwa kwayo. (MWANZO 3:1-21)  Mwanzo 3:9 "BWANA MUNGU AKAMWITA ADAMU, AKAMWAMBIA UKO WAPI? ni sauti ya Mungu inasikika baada ya mwanadamu kutenda uasi.  
  3. Wanadamu wote tu wazao wa Adamu, hivyo baada ya Adamu,  wanadamu wote tumezaliwa katika sura ya Adamu, kila anayezaliwa anazaliwa katika dhambi.                MWANZO 5:3 "Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa SURA YAKE, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.  Hivyo hakuna aliye salama, WATU WOTE TUNAMWITAJI YESU, WAKUBWA KWA WADOGO!   Injili ni lazima. 
  4. Mwanadamu amekuwa nje ya Mungu kwa mda mrefu sana, hivyo mwanadamu ametumikia giza na kufikia hatua ya  kupenda giza kuliko NURU.                         (YOHANA 3:19) "Na hii ndyo hukumu;ya kuwa Nuru imekuja ulimwenguni,  na watu wakapenda giza kuliko nuru;kwa maana matendo yao yalikuwa maovu"  (TUNAHITAJI KUHUBIRI HABARI ZA YESU AMBAYE NI NURU ILI KILA MTU AJUE HABARI HIZI) 
  5. Hakuna njia nyingine zaidi kwa mwanadamu mtenda dhambi na muasi kuweza kuwa na mahusiano na MUNGU  MTAKATIFU NA MWENYE HAKI.   Njia pekee ni kupeleka Habari Njema za TOBA NA MSAMAHA WA MUNGU, kwa sababu ni TOBA YA KWELI kwa njia ya DAMU YA YESU ambayo hutupatanisha Kwa Mungu na kurudisha USHIRIKA WETU PAMOJA NA MUNGU BABA. 
C:HALI YA MWANADAMU NJE YA YESU KRISTO! (NJE YA NEEMA YA WOKOVU
  • Watu wote ni wenye dhambi na wako chini ya Hukumu ya Kifo.                               Warumi 5:12" Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi ilingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti;na hivuo mauti ikawafakianwatu wote kwa sababu watu wote wamefanya dhambi"    WARUMI 3:21 "Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu"  waebrania 9:27.

  • Watu wote wanahesbiwa kuwa wamekufa kwa sababu ya makosa na dhambi.   WAEFESO 2:1 "Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu" Dhambi husababisha Kifo cha kiroho, kuondoka kwa Roho mtakatifu na kifo cha kimwili. 
  • Watu wote ni watoto wa Hasira  na huenenda kwa tamaa za kimwili. WAEFESO 2:3.

  • Watu wote wamefarakana na kuwa mbali na uzima wa MUNGU. WAEFESO 4:17-18..

  • Watu wote wema, waungwana na wenye kutenda mema WANAITAJI KUOKOLEWA. Warumi 3:23,Wote wamefanya dhambi, YOHANA 3:3 "YESU AKAJIBU, AKAMWAMBIA, AMIN, AMINI, NAKUAMBIA, MTI ASIPOZALIWA MARA YA PULA, HAWEZI KUUOONA UFALME WAA MUNGU"

  • Watu wote wasio mpokea Yesu na kurudi katika mahusiano mazuri na Mungu, WAMEWEKEWA HUKUMU YA MILELE AMBAYO NI UHARIBIFU NA ADHABU KATIKA JEHANAMU YA MOTO. (UFUNUO 20:10-15). 
🎤HIVYO, INJILI INAHITAJIKA KWA HARAKA SANA KWA WATU WOTE, ILI KULITIMIZA KUSUDI  LA MUNGU  AMBAYE ANATAMNI WATU  WOTE WAOKOLEWE... LET US GO, GO, GO AND PREACH THE GOOO NEWS OF SALVATION. 

D: HABARI NJEMA NI NII(Wahat is the "Good News) 

➕Mungu aliamua kumrudisha mwanadamu tena katika Mahusiano yake KWA KUMTUMA YESU KRISTO KUWA MWOKOZI WA ULIMWENGU (Mwanzo 3:26-29),YOHANA 3:16, YOHANA 1:12. Hivyo Mwanadamu amepewa nafasi nyingine katika Ufalme wa Mungu, Ya kuwa Mwana wa Mungu na Raia wa ufalme wa Mungu. Mtu anapomwamini Bwana Yesu  anafanyika MWANA KATIKA UFALME WA MBINGUNI. 

1.Yesu pia ni sura ya Mungu (Waebrania 1:3).
2.Yesu hakutenda Dhambi kama Adamu. (Waebarnia 4:15)
3.Yesu amebeba na kuchukua Dhambi zetu. 

 WARUMI 5:8 "BALI MUNGU AONYESHA PENDO LAKE YEBMWENYWE KWETU SISI, KWA KUWA KRISTO ALIKUFA KWA AJILI YETU, TULIPOKUWA TUNGALI WENYE DAHMBI" 

➕WOTE WANAOMPOKEA KRSTO KAMA MWOKOZI, WANAKUBALI KAZI ILIYOMALIZIKA PALE CALVARY MSALABAINI kama NJIANPEKEE YA WOKOVU, wanatubu dhambi zao na Kukiri Kuws Yesu ni Bwana na wanazliwa katika Krsto na kufanyika WATOTAO WA MUNGU. Yohana 3:1-5.
YOHANA 14:6 "YESU AKAMWAMBI, MIMI NDIMI NJIA, NA KWELI NA UZIMA;MTU HAJI KWA BABA, ILA KWA NJIA YA MIMI"

1.Tunahesabiwa kuwa na HAKI kwa njia ya KUMWAMINI YESU TU. (Warumi 4:5,22-25)
2.HAKUNA HUKUMU KWA WALIO KATIKA YESU. WARUMI 8:1-2.
3.TUNAPATA TENA SURABYA MUNGU KWA NJIA YA YESU KRISTO(Tunakuwa Raia wa mbinguni TENA) Waebrania 8:28-30.
4.TUNAPATA AMANI KATIKA KRISTO YESU. (WARUMI 5:1)"Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. "
5.TUNAPATA UHURU WA KWENDA KWA BABA MUNGU kwa njia ya Yesu Kristo.                       WARUMI 5:2.

➕Mwanadamu anarudishwa katika USHIRIKA KAMILI WA BABA NA KUWA WASHIRIKA WA  UTUKUFU WA UTAJIRI WA MUNGU. (Ephesia 1:18,Wakolosai1:27,Roma 9:23).

➕MUNGU AMETOA NJIA MOJA YA WOKOVU KWA WANADAMU WOTE, wayahudi na wa mataifa. (warumi 3:10,5:21.) NI YESU KRISTO PEKEE AMETOLEWA NA  MUNGU KUWA MWOKOZI WA ULIMWENGU. 

E: NANI MWENYE JUKUMU LA KUHUBIRI HABARI NJEMA KWA ULIMWENGU?? 

  1. KANISA LA KRISTO, kuanzia Mwamini mmoja na watu wote. Mathayo 16:18,1petro 1:12.MUNGUhufanya kazi yake kupitia watu wake. 
  2. Ujumbe wa INJILI LAZIMA UHUBIRIWE KUPITIA SAUTI ZA WATU WA MUNGU(WARUMI 10:13-15)
  3. KANISA au WAAMINI NI LAZIMA KUUFIKIA ULIMWENGUna watu wote Kabla ya KURUDIBKWA YESU MARABYA PILI, kwa sababu baada ya hapo HAKUNA NAFASI NYINGINE. (2Wathesalonike 4:13-18)
  4. KANISA lisipofanya kazi ya INJILI YA YESU, haitaweza kufanyika. (Waefeso 3:8-12).HIVYO NI MUHIMU KANISA TUONDOKE NA KUHUBIRI HABARI HIZI NJEMA KWA WATU WA MUNGU. 
🎤MATHATO 24:14 "TENA HABARI NJEMA YA UFALME ITAHUBIRIWA KATIKA ULIMWENGU WOTE, KUWABUSHUHUDA KWA MATAIFA YOTE, HAPO NDIPO MWISHO UTAKAPOKUJA" 
Imetupasa kuhubiri.. Habari hizi.. Ambazo ni TOBA NA MSAMAHA WA DHAMBI KWA WANADAMU KWA NJIA YA YESU KRISTO. 

F: NI MAANA YA KUWA MSHUHUDIAJI WA HABARI NJEMA? ( TO BE A WITNESS) 
  1. Kuwa tayari kutoa ushuhuda wa yale uliyoona na kushudia na kusikia. 1Yohana 1:1-4.
  2. Kuishi maisha yanayoedena na Ukiri wako WA WOKOVU.  Maisha ya kumfuata Bwana Yesu Kristo. 1Wakorinto 11:1.
  3. Kuishi maisha ya NURU kupitia KUTENDA MATENDO MEMA kwa wati na kwa Mungu pia (KUMPENDEZA MUNGU NA WANADAMU PIA),  Saidia watu, zungumza  kama Mwana wa Mungu,  Be Honest. 
  4. Ni kuzungumza na kushirikisha habari njema kwa watu popote, nafasi inapofungiwa. LUKA 21:13.

G:VITU MUHIMU KATIKA HUDUMA HII VYA KUFAHAMU! NA KUZINGATIA. 

  1. YESU YUPO PAMOJA NASI SIKU ZOTE.   Muhimu ni sisi KUKAA NDANI YAKE. MATHAYO 28:20b, "NA TAZAMA, MIMI NIPO PAMOJA NANYI SIKU ZOTE, HATA UKAMILIFU WA DAHARI"                                                                                              YOHANA 15:5 "Mimi ni mzabibu;ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana;MAANA PASIPO MIMI NINYI HAMWEZI KUFANYA NENO LOLOTE" 
  2. ROHO MTAKATIFU NI MTU MUHIMU SANA KATIKA KAZI HII YA INJILI. Hivyo tunamwitaji  ROHO MTAKATIFU, kwa ajili ya  kutupa NGUVU YA KUPELEKA INJILI KILA MAHALI... Naye YUPO PAMOJA NASI MILELE.    MATENDO YA MITUME 1:8 "Lakini mtapokea nguvu,  akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashaidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote,  na samaria,  na hata mwisho wa nchi"
  3. KUWA NA IMANI KATIKA MUNGU, YESU NA ROHO MTAKATIFI, Tukijua ya kuwa anayeokoa  na kutenda ni MUNGU.                                                                             YOHANA 14:12 "Amini, amin, nawambia, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam na kubwa kulikobhizo atafanya,  kwankuwa miki naenda kwa Baba. 
  4. KUHUBIRI NA KUZUNGUMZA KUSUDI LA MUNGU(Ni muhimu sana kujua na kuyazungimza Mapenzi ya Mungu kwa watu wake na si matakwa yetu)   MATENDO YA MITUME 20:27 "KWA SABABU SIKUJEEPUSHA NA KUWAHUBIRIA HABARI YA KUSUDI LOTE LA MUNGU"   Ni muhimu sana, tuhubiri KIINI KIKUBWA CHA KUJA KWA YESU AMBACHO NI WOKOVU WA MWANADU! 
  5. YOTE YAFANYIKAYO,  UTUKUFU WOTE TUNAMPA MUNGU AMBAYE NDIYE ANAYEOKOA, ANAPONYA, ANATENDA MAAJABU. Sisi ni watumishi wake tu, na imetupasa kufanya hivyo.                 .            .  .... .                                                        
  6. FAHAMU KUWA MUNGU KIU YAKE NA MOYO WAKE ATAKA WATU WOTE WAOKOLEWE. 

🎤1TIMETHEO 2:1-6,  3 "HILO NI ZURI, NALO LAKUBALIKA MBELE ZA MUNGU MWOKOZI WETU, AMABAYE HUTAKA WATU WOTE WAOKOLEWE, NA KUPATA KUJUA YALIYO KWELI"  KWA SABABU MUNGU NI MMOJA, NA MPATANISHI KATI YA MUNGU NA WANADAMU NI MMOJA, MWANADAMU KRISTO YESU"

Ubariwe sana kwa kufuatilia somo hili,  unaweza kufuatilia masomo. Mengine pia kupitia blog hii. 

Be blessed. JESUS LOVES YOU SO MUCH THAT HE DIED ON THE CROSS FOR US!! LET US GO, GO, GO AND SPEAK GOOD NEWS TO ALL PEOLE. 
Jemrath bikombo. Jbrev@0753775948.


Monday, 24 July 2017

UWAKILI WA MUNGU (STERWARDSHIP OF GOD)


  • Hellow watu wa MUNGU, nakukaribisha katika blog hii ambayo unapata masomo mbalimbali kuhusu UFALME WA MUNGU na Maisha yako. Ubarikiwe sana. Karibuni sana.


SOMO :UWAKILI WA MUNGU.  SISI NA VITU VYOTE NI MALI YA BWANA.

Mwanzo 1:1 " HAPO MWANZO MUNGU ALIZIUMBA MBINGU NA NCHI"   MUNGU ndiye mmiliki wa kila kitu, aliyeumba, NDIYE ANAYEMILIKI VITU VYOTE!
ZABURI 24 :1 "NCHI NA VYOTE VIIJAZAVYO NI MALI YA BWANA, DUNIA NA WOTE WAKAAO NDANI YAKE" 


A. MAANA YA WAKILI : Ni mtu aliyepewa dhamana juu ya mali ya mtu mwingine! 

KUMBUKA, katika kitabu cha MWANZO 1:28-31. Mungu MUUMBA alitukabidhi mali yake ili tuitunze kwa UTUKUFU wake.
WAKILI (manager, steward, administrator).


  • UWAKILI unaonyesha mahusiaano makubwa kati ya Mungu na Mwanadamu.  "GOD as a OWNER and Man as a MANAGER"

MUNGU ametuweka sisi kuvisimamia vitu vyote tulivyo navyo katika maisha yetu. (it is a DIVINE TRUST).

SIFA KUU ZA MAWAKILI AMBAO MUNGU ANATAFUTA. 
1.MAWAKILI WAAMINIFU.
2.MAWAKILI WENYE BUSARA.

  • WAKILI MWAMINIFU ni yule anayetambua kwamba yeye na vitu alivyonavyo ni MALI YA MUNGU. Pia huishi na kutumia vyote kwa ajili ya MUNGU. 

  • WAKILI Mwenye BUSARA huilinda mali ya BWANA wake na kuendelea kuzalisha na kuzaa matunda mpaka BWANA wake ATAKAPOKUJA, hakati tamaa, NI mvumilivu. Anawajibika kwa mali ya BWANA wake. (LUKA 12:42-48). 

MATHAYO 25 :14 - 30. (WATUMISHI waliopewa TALANTA).


  1. HAGAI 2:8 "Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, ASEMA BWANA wa MAJESHI. 
  2. ACTS 17 :25" Kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na Pumzi yangu, ASEMA BWANA "
SISI sio wamiliki wa maisha yetu na vitu vyetu, MUNGU ametuweka kuwa MAWAKILI WAKE. 1WAKORINTO 4:1-2" Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa KRISTO na MAWAKILI wa siri za MUNGU. Hapo tena inayohitajiwa katika MAWAKILI, ndiyo Mtu aonekane kuwa MWAMINIFU "

N.B :WAKILI MWEMA anafanya mambo yote kwa faida na HESHIMA na UTUKUFU WA BWANA WAKE.

B:MAENEO YETU YA UWAKILI, AMBAYO MUNGU AMETUPA!

  1. UWAKILI WA MUDA WETU. Muda ni  kitu cha muhimu Sana, kwa sababu muda ukipita umepita, haujirudii tena. Tunapaswa kutumia mda wetu vizuri kwa UTUKUFU wa MUNGU.                                                                                                                                  Pia tunahitaji kutumia muda wetu vizuri kwa ajili ya HUDUMA, KAZI, FAMILIA., Masomo.  1PETRO 4:2.    , 1 korinto 10:31.                                                                Waefeso 5:15-16 "MKIUKOMBOA WAKATI KWA MAANA ZAMANI HIZI NI ZA UOVU".
Tusitumie mda huu mchache tuliopewa na MUNGU duniani kufanya yasiyo mpendeza, bali TAFUTA KUYAFANYA MAPENZI YA MUNGU kila mda, Pangilia mda wako na TUMIA MDA HUU KUYAANDAA MAISHA YAKO YA MILELE. Baada Ya mda huu hatutapata mda . Mwingine. 
     2. UWAKILI WA MIILI YETU. 

  • Tumeumbwa kwa sura na mfano wa MUNGU. 
  • Mungu anaagiza tuitoe miili yetu iwe dhabihu na kuifanya ibada. 
  • Tunapaswa kumpenda MUNGU kupitia miili yetu.  WARUMI 12:1. 
  • Miili yetu ni mahekalu ya ROHO MTAKATIFU. 1 korinto 3:16 " au hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hakalu la ROHO MTAKATIFU na ya kuwa Roho wa anakaa ndani yenu?. 
  • Kuishi maisha matakatifu na kujitenga na dunia na kumkaribia MUNGU. 
  • Hatupaswi kuitumia miili yetu kwa dhambi na uovu.   
  • Pia MUNGU anatamani tuitunze miili yetu na afya zetu,, kula vizuri, PUMZIKA, fanya mazoezi. 
  • Tuishi kwa ajili ya MUNGU tu 1.Kumuabudu 2.Kumtii 3.Kuwa HAI katika Bwana na kufa kwa habari ya dhambi. 
          3.UWAKILI WA MALI ZETU. 
"KUTOKA 19 :5 "Maana dunia yote ni mali yangu"   Tukumbuke kwamba ndiye  anaayetupa mali na vitu vyote tulivyo navyo. Tunapaswa kuvitumia kueneza UFALME WAKE

AYUBU 41 :11 "Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe? Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni CHANGU" 
MUNGU anaagiza tutumie mali tulizopewa kwa ajili ya UTUKUFU wake, mfano, Nyumba, gari, Ardhi. 

         4.UWAKILI WA KARAMA, VIPAWA, TAALUMA NA HUDUMA
MFANO, Uimbaji, karama za ROHONI, Udaktari, Ualimu, komputya, ufundi umeme, na kila Kazi yoyote unayofanya. 
Vyote hivyo, MUNGU amekupa kwa ajili ya kutumika Kuujenga UFALME WAKE UNAVITAWALA.. WAEFESO 4:11 - 16. 

5.UWAKILI WA FEDHA ZETU NA UTAJIRI
Mungu ametupa fedha kwa ajili ya UTUKUFU wake na kueneza Kazi yake. KURUDI la Mungu kuhusu Fedha ni kuwabariki Watoto wake, kutuwezesha Kuishi maisha yenye BARAKA KWA kujifunza KUTOA NA KUPOKEA!

KWA NINI TUTOE FEDHA ZETU.

  1. BIBLIA TAKATIFU INATUFUNDISHA UTOAJI (malaki 3:8-12) 
  2. NI AGIZO LA YESU (LUKA 6:8) 
  3. TUNAONYESHA UPENDO WETU KWA MUNGU (1 korinto 13 :4)
  4. TUNAWEKA HAZINA KWA MUNGU. 
  5. NI HERI KUTOA KULIKO KUPOKEA Acts 20:35). 
  6. KRISTO mwenyewe ALIJITOA kama sadaka kwa ajili yetu. 
  7. KWA AJILI YA KUENEZA UFALME WA MUNGU NA KAZI YA MUNGU DUNIANI. 
  8. Tunapaswa kumtolea MUNGU kwa HIARI, FURAHA, UTIIFU, UHURU, UWIANO, UKARIMU NA KWA DHABIHU. 
  9. Tukumbuke kumtolea MUNGU ZAKA (FUNGU LA KUMI) MWANZO 14 :18-20) SADAKA inayonyesha kwamba MUNGU NDIYE ANAYEMILIKI. 
    C: FOUR PRINCIPLES OF STEWARDSHIP!

THE FUNDAMENTAL PRINCIPLE OF ALL PEOPLE States that " we own nothing, God owns everything, we are simply managers "

1.THE PRINCIPLE OF OWNERSHIP (UMILIKI) Genesis 1:1,ZABURI 24. God created everything, He only owns everything.

2.THE PRINCIPLE OF RESPONSIBILITY (UWAJIBIKAJI). Mungu ana HAKI ya UMILIKI, MAWAKILI wana wajibika. Mungu ametuita kusimamia MALI yake,Tunapaswa kuwajibika.

3.THE PRINCIPLE OF ACCOUNTABILITY. (KUTOA HESABU)   WARUMI 14 :12 "Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za MUNGU"
Tutatoa HESABU ya vile tilivyokabidhiwa (Time, money, ability, information, wisdom, authority, talents, work Education, relationship, resources and opportunities).

4.THE PRINCIPLE OF REWARD ( MALIPO).  
MATHAYO 25 :21 "BWANA wake akamwambia, vema, mtumwa mwema na MWAMINIFU, ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya Mengi, ingia katika FURAHA YA BWANA wako"
Wakolosai 3:23 - 24.

MUHIMU SANA :"There is no greater choice offered to us than surrender to the one who CREATED us and knows us better than we know ourselves "

SWALI LA KUKUMBUKA :LUKA 18 :8  " WALAKINI, ATAKAPOKUJA MWANA WA ADAMU, JE, ATAIONA IMANI DUNIANI?

ubarikiwe sana kwa kujifunza. UTUKUFU KWA MWOKOZI YESU KRISTO ANAYEOKOA NA KUTUPA ROHO MTAKATIFU KUTOKA KWA MUNGU BABA. Amen.

Jemrath Bikombo.

Friday, 21 April 2017

SIRI SABA ZA MAISHA (UKIWA HAI) (GOD REMAINS GOD FOREVER)

BWANA Yesu KRISTO MWOKOZI PEKEE APEWE SIFA. Ninakukaribisha tena katika blog hii, ILI uweze kujifunza masomo mbalimbali kuhusu UFALME WA MUNGU.

SOMO :ZIFAHAMU SIRI ZA MAISHA, ILI UISHI KWA AMANI BILA MAWAZO NA MASWALI MENGI (UNDERSTAND THE SECRETS OF LIFE, IN ORDER TO REDUCE CONFLICTS, STRESS, DEPRESSIONS AND PROBLEMS) IN YOUR LIFE!

   NENO LA MUNGU :KUMBUKUMBU LA TORATI 29:29
"MAMBO YA SIRI NI YA BWANA, MUNGU WETU, LAKINI MAMBO YALIYOFUNULIWA NI YETU SISI NA WATOTO WETU MILELE, ILI TUYAFANYE MANENO YOTE YA SHERIA HII"
AYUBU 38 - 42. (Soma hizi sura, BWANA ANAZUNGUMZA MAAJABU YAKE)
AYUBU 40 :2a."
Je!Mwenye hoja atashindana na MWENYEZI?
YEREMIA 23 :23 - 24 
"Mimi ni Mungu aliye karibu, asema BWANA, mimi si Mungu aliye mbali. JE, mtu ye yote aweza KUJIFICHA mahali pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema BWANA.

WARUMI 11 :33 - 36
" Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya MUNGU! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani" Maana ni nani aliyeijua nia ya BWANA? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake? Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena?
KWA KUWA VITU VYOTE VYATOKA KWAKE, VIKO KWA UWEZA WAKE, TENA VINAREJEA KWAKE. UTUKUFU una YEYE MILELE. AMINA.

     Rafiki, mpendwa, ndugu msomaji , MAISHA (KUISHI)UHAI  ni ZAWADI KUTOKA KWA MUNGU anayotupa kwa ajili ya KUSUDI lake maalum na kwa wakati maalum. (LIFE  IS A GIFT FROM GOD)
       
NOTE THE FOLLOWING BELOW!

  • LIFE WITH  A PURPOSE HAS MEANING! 
  • LIFE WITHOUT PURPOSE HAS NO MEANING! 
  • LIFE WITH GOD HAS MEANING! 
  • LIFE WITH GOD, HELP YOU DISCOVER YOUR PURPOSE! 
  • THE PURPOSE IS CLOSED IN CERTAIN TIME, PERIOD OR SEASON! 
  • DISCOVERING YOUR PURPOSE IS IMPORTANT because TIME is not waiting You! 
  • ONLY YOUR PURPOSE, CAN MAKE YOU ENJOY YOUR LIFE! 
  • WE ARE BORN UNIQUE, ORIGIN, IN IMAGE OF GOD! - Find your value in God, GOD is within us.. Find likeliness of GOD IN YOUR LIFE! 
  • DON'T COPY AND PASTE OTHER'S LIFE INTO YOUR LIFE!... ... You may create a lot of stress and problems. 
  • LIFE GOES WITH FAITH... Extraordinary FAITH, TRUSTING LORD for all! 
  • LIFE WITHOUT FAITH HAS NO MEANING, because there is no HOPE.
Only God's Kingdom FAITH in JESUS CHRIST IS the ANSWER to all, questions  problems, stress, tests and temptations! 

  SEVEN SECRETS /MYSTREIS OF LIFE!

  1. There are QUESTIONS in LIFE we can never answer!. .answer only what you know, don't try to answer every questions comes into  your life. 
  2. There are THINGS in LIFE we can never explain... When you try to explain everything, you can create your self explanation... Explain only what you can.  
  3. There are THINGS in LIFE we can never change...Change may come as the time fulfill! 
  4. There are THINGS in LIFE we can not control... just to let them go and pass! 
  5. There are THINGS in LIFE we can not stop..... . . Create a way for them to move on, allow peace in your life. Example. You can't stop death. 
  6. There are THINGS in LIFE we are NOT Responsible for.... Know what you are responsible for, do it.
  7. There are THINGS in LIFE we cannot EXCEED..(Two words are important here (YES or I DON'T KNOW).
 IMPORTANT KEY TO LIFE!

  • Know  your limitation! 
  • Know your responsibility (purpose created for on earth) 
  • Know what is not your responsibility. 
  • Example, we are responsible for Controlling our will.(control your will to Eternal LIFE) 
  • Know what you can do and what you cannot do! 
  • Life on earth is temporary, don't make a permanent solution to worldly things! 
  • Life after earth is ETERNAL, hence Make a blessed Choice or permanent nice solution to get ETERNAL LIFE.. by ACCEPTING AND RECEIVING JESUS CHRIST AS YOUR SAVIOUR in your LIFE! Be blessed! 
IMPORTANT Five QUESTIONS   EVERYONE IS FINDING IN LIFE ON EARTH! 

  1. WHO I AM? - VALUE & IDENTITY! 
  2. WHERE ARE I AM FROM?  - Heritage! 
  3. WHY I AM HERE FOR?  - PURPOSE! 
  4. WHAT CAN I DO? - POTENTIAL! 
  5. WHERE I AM GOING? - Destination, Eternity, HOPE! 
JIBU LA MASWALI HAYO LINAPATIKANA "

MWANZO 1:26 - 30 
" MUNGU akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi "
" MUNGU akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa MUNGU alimwumba, mwanamme na mwanamke aliwaumba "

YOHANA 1 :12-13.
BALI WOTE WALIOMPOKEA ALIWAPA UWEZO WA KUFANYIKA WATOTO WA MUNGU, NDIO WALE WALIAMINILO JINA LAKE,

YOHANA 14 :1 - 2.
Msifadhaike mioyoni mwenu, mnamwamini MUNGU, niaminini na Mimi. Nyumbani mwa BABA yangu mna makao mengi, kama sivyo, ningaliwaambia, Maana naenda kuwaandalia mahali.

NOTE THE LAST IMPORTANT sentence BELOW!
(MWACHE MUNGU ABAKIE KUWA MUNGU PEKEE)
LET GOD BE GOD!

  • There are Things ONLY GOD CAN DO! 
  • There are Things ONLY GOD KNOWS! 
  • There are Things ONLY GOD UNDERSTANDS! 
  • There are Things ONLY GOD CAN EXPLAIN! 
  •     ZABURI 89 :6 
  • "Maana ni nani katika mbingu awezaye kulinganishwa na BWANA? Ni nani afananaye na BWANA miongoni mwa malaika? 
  • ZABURI 89 :11 
  • "MBINGU NI MALI YAKO, NCHI NAYO NI MALI YAKO, ULIMWENGU NA VYOTE VIIUJAZO NDIWE ULIYEUPIGA MSINGI WAKE! 
Ubarikiwe sana ndugu msomaji, ROHO MTAKATIFU akujaze maarifa ya Mungu!
KUMBUKA!
YOHANA 14:6 YESU AKAMWAMBIA, MIMI NDIMI NJIA, NA KWELI, NA UZIMA, MTU HAJI KWA BABA, ILA KWA NJIA YA MIMI.
        Father GOD, JESUS CHRIST and HOLY SPIRIT love  you so much, they have come now on earth to return us into our Original Home, receive them and get back your ETERNAL LIFE!
Reference from Dr. Myles munroe, Rev. Rick warren. 
By JEMRATH BIKOMBO. Jbrev@! 


Friday, 24 March 2017

IBADA YA KWELI MBELE ZA MUNGU BABA.

 Nawasalimu katika jina la MUNGU  BABA, MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO MTAKATIFU.
 Karibuni tena tuendelee kujifunza habari za UFALME WA MUNGU. 

SOMO :IBADA YA KWELI MBELE ZA MUNGU. 
  
  Utangulizi, NENO KUABUDU linaoneka kwa mara ya kwanza katika MWANZO 22 :5 "Ibrahimu akawambia vijana wake, kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, TUKAABUDU, na kuwarudia tena" 

MAANA YA IBADA ni hali ya Moyo wa mwanadamu kuwa na USHIRIKA NA MUNGU. 
MOYO wa mwanadamu umeumbiwa na una Hulka ya KUFANYA IBADA. Pia kusudi la Mungu kumwumba mwanadamu ni ILI awe na USHIRIKA naye. 

Yohana 4:23 - 24 "Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabudio halisi wstamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 
Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli" 

    IBADA YA KWELI HUHUSISHA :
  1. MUNGU. 
  2. MWANADAMU. 
  3. MADHABAHU (MOYO), 1Falme 18 :30. 
  4. ROHO MTAKATIFU. MATHAYO 18:19-20 
  5. UTAKATIFU. 
  MADHABAHU YA KWELI NI MOYO WAKO - mahali ambapo MUNGU na mtu hukutana. 
Mwanadamu, baada Ya kuokoka, ROHO MTAKATIFU anaingia ndani ya mtu na kuanza Kuishi naye. 
Hivyo, MTU hufanyika kuwa HEKALU LA MUNGU.
  •  1 wakorinto 6:19 - 20 
  • Rumi 12:1 
@Madhabahu (MOYO wako) inatakiwa kuwa 
  • NI mahali pa dhabihu (kujitoa mbele za MUNGU) 
  • Ni mahali pa kujikana (kuacha vitu vyote, shughuli zote, unavyovipenda, n.k. (UNAKUBALI NA KUMPA MUNGU NAFASI  YA KWANZA maishani mwako) 
  • Ni mahali pa moto (sehemu inahitajiwa kutunzwa siku zote na mda wote. MITHALI 4':23 "Linda Moyo wako kuliko yote uyalindayo, Maana ndiko zitokako  chemchemi za uzima" 
  • Ni mahali pa kiu na njaa ya HAKI ya kukutana na MUNGU. 
UMUHIMU WA KUWA NA IBADA MAISHANI MWAKO. 
@UNAKUWA MALI YA MUNGU 
@UNAKUWA NA USALAMA 
@UPENDO WA MUNGU UZALIWA NA KUACHILIWA MAISHANI MWAKO. 
UTAFANYIKA BARAKA KWA WATU, JAMII NA TAIFA KWA UJUMLA. 

MAMBO YA MUHIMU NA KUKUMBUKA ZAIDI. 
  1. Madhabahu (MOYO) ni sehemu muhimu katika maisha ya IBADA. 
  2. MADHABAHU (MOYO) ni sehemu muhimu katika USHIRIKA NA MUNGU. 
  3. NI wajibu wa mtu kuandaa madhabahu yake katika MAISHA ya IBADA. 
  4. MADHABAHU ni sehemu inayopaswa kutoa Harufu nzuri, safi na ya KUMPENDEZA BWANA. 
  5. Madhabahu lazima itunzwe siku zote (MAOMBI, NENO) 
  6. MADHABAHU isipotunzwa, mtu hatafurahia uzuri wa IBADA. 
  7. MOYO UKIWA HAI KWENYE MAISHA kYA IBADA NA MUNGU, UNATENGENEZA MAISHA NA HATIMA ILIYO HAI. 
  8. ROHO MTAKATIFU ni mtu muhimu sana katika maisha ya IBADA (hutuongoza, hutufariji, hutufundisha neno, hutupa siri za MUNGU, hututia nguvu) 
  9. Ni wajibu wa mtu, kutambua UMUHIMU WA ROHO MTAKATIFU, na kumshirikisha katika maisha yetu ya kila siku. 
  10. IBADA YA KWELI NA YA PEKEE NI KUMWABUDU MUUMBA WETU ALIYETUUMBA. 

   Pia, ibada huambatana na SIFA, NYIMBO, TENZI, KUSUJUDU, SADAKA, NENO. 
"
         "HAZINA YAKO ILIPO, NDIPO NA MOYO WAKO UTAKAPOKUWA 
 MUNGU BABA WA MBINGUNI awabarki sana, karibuni tena. 

Wednesday, 15 March 2017

FAHAMU UNDANI WA KWA NINI YESU ILIBIDI AJE NA KUFA ILI KUTUOKOA.

Rafiki, ndugu na mpendwa, nakusalimu katika JINA LA MUNGU BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU.
   Napenda kukukaribisha katika somo hili, ili Tuweze kujifunza ZAIDI kuhusu UFALME WA MUNGU.

SOMO : KWA NINI YESU ILIBIDI AJE NA KUFA MSALABANI ILI KUTUOKOA MIMI NA WEWE? 
   
YESU KRISTO ni mtu aliyewahi Kuishi hapa duniani, na kuacha HISTORIA mpaka leo, kutokea miaka 2000 iliyopita. Ni mtu Pekee ambaye jina lake, kazi zake na ujumbe wake vinatajwa hata leo kuliko mtu mwingine aliyewahi Kuishi hapa duniani. 

VITU AMBAVYO BADO VINATAJWA KUHUSU YESU KRISTO LEO. 

  1. KUZALIWA KWAKE, alivyozaliwa kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU kupitia Mariamu Bikira.
  2. MAISHA YA YESU, Maisha bila dhambi, miujiza yake. 
  3. UJUMBE WA YESU KUHUSU UFALME WA MUNGU, alitangaza msamaha wa dhambi, uzima wa MILELE. Upendo WA MUNGU BABA. 
  4. KIFO CHA YESU, jinsi alivyokufa, kwa nini alikufa, nani alimuua. 
  5. KUZIKWA KWAKE (KABURI ALILOZIKWA) 
  6. KUFUFUKA KWA YESU KRISTO, jinsi alivyofufuka na kwa nini ilibidi afufuke. 
  7. KURUDI KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI, ni wakati gani atarudi na kwa nini.
   Hivyo ni baadhi ya vitu vinavyoleta maswali kwa wengi, KUHUSU YESU KRISTO MWOKOZI. Watu wengi wakiwemo wasomi, wanasayansi, wanafilosofi, atheists, religious people, wamebaki bila majibu kuhusu HUYU YESU KRISTO, Wengine wakisema alikuwa mtu wa kawaida, mtu mwema,n.k. WAKIKATAA UKWELI ULIO WAZI. 

 TUANGALIE SASA KWA NINI YESU KRISTO, DUNIANI.
Tuangalie vipengele vifutavyo kwanza kabla ya kwenda ndani ZAIDI, tujue mwanzo wa YOTE haya!

KUUMBWA KWA MWANADAMU, Mwanzo 1:27 "MUNGU AKAUMBA MTU KWA MFANO   WAKE, KWA MFANO WA MUNGU ALIMWUMBA, MWANAMME NA MWANAMKE ALIWAUMBA"    Mwanzo 2:7, MUNGU alituumba kwa mfano wake, lengo lake tuweze kumwakilisha katika ULIMWENGU ili kuutunza UTUKUFU wake, MUNGU alupoumba vitu vyote aliviumba kwa UTUKUFU WAKE.                                                        ASILI yetu tokea Mwanzo ni MBINGUNI, UASI ulifanya tupoteze asili yetu ya MBINGUNI.  MUNGU alipoumba vitu na mwanadamu, alimpa mwanadamu MAMLAKA ya KUVITAWALA na kuvitunza, hiyo yote MUNGU, lengo lake ni kutushirikisha UTUKUFU wake katika UFALME WA MUNGU. 

2.CHANZO CHA KIFO(MAUTI) , DHAMBI.  MWANZO 2:16-17 "BWANA MUNGU akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mtu wa bustani waweza kula, Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo UTAKUFA HAKIKA"
  •   AGIZO LA MUNGU kwa MTU linahusisha vitu vitatu muhimu :1 . MTU 2.MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA 3.KIFO (UTAKUFA(MAUTI ). Fahamu yafautayo ni muhimu :
  • MUNGU aliumba KIFO. (MAUTI) 
  • KIFO kilikuwepo hata kabla hakijaanza kuua. 
  • KIFO kiliumbwa kikiwa hakina nguvu ya kuua (kiliumbwa kikiwa hakifanyi Kazi) 
  • KIFO kiliumbwa kikiwa hakina UHAI. 
  • Mauti iliumbwa bila tatizo (Normal). 
  • MUNGU alimwambia MTU siku utakapokula Tunda LA Mti wa ujuzi wa mema na mabaya, UTAKUFA, MTU alikuwa na uwezo wa kuchagua KIFO au kuendelea KUISHI katika BUSTANI YA EDENI. 

  • KUMBUKUMBU LA TORATI 30:19-20 "Nazishuhudiza mbingu na nchi hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako UZIMA NA MAUTI, baraka na laana, BASI chagau UZIMA ili uwe hai, wewe na uzao wako, KUMPENDA BWANA, MUNGU, WAKO, KUITII SAUTI YAKE, NA KUSHIKAMANA NAYE, KWANI HIYO NDIYO UZIMA WAKO, NA WINGI WA SIKU ZAKO, UPATE KUKAA KATIKA nchi BWANA aliyaowaapia baba zako, Ibrahim na Isaka na Yakobo, kuwa atawapa "
DHAMBI NA KIFO BAADA YA UASI. 
           DHAMBI ni uasi dhidi ya amri ya  MUNGU (REBELLION AGAINST THE WILL OF GOD) or TO MISS OUT the PRESENCE OF GOD. 

Dhambi ya mtu katika bustani ya Edeni ilikipa KIFO uwezo wa kufanya Kazi na kuanza Kuua tangu wakati huo, KIFO ni matokeo ya dhambi, kutotii amri ya Mungu (DISOBEDIENCE OF GOD'S WORD). 
Baada Ya dhambi Mauti ikawa na tatizo (abnormal) ikaanza kuua. 

Dhambi ya ADAMU, ikakipa ruhusa KIFO kuua.

NINI MAANA YA KIFO (MAUTI)
1.Kuondoka kwa ROHO MTAKATIFU katika maisha ya mtu (Very dangerous) (departure of HOLY SPIRIT, leaving man spirit) 
2.KUTOKA KATIKA UWEPO WA MUNGU (departure of Man in presence of GOD) 
3.Kuondoka kwa Roho ya mtu (departure of Man spirit, leaving human being). 

Note :Tangu siku ile mtu alipokula matunda, alipoasi Amri ya MUNGU, alikufa siku hiyo , japo aliendelea Kuishi kwa maisha ya nje, Na Vizazi vyote vilivyofuatia vilizaliwa katika dhambi hiyo. 
Pia, MUNGU hakumuua Adamu BALI KIFO (MAUTI) kilimuua Adamu. 

WARUMI 5:12 "KWA HIYO, KAMA KWA MTU MMOJA DHAMBI ILIINGIA ULIMWENGUNI, NA KWA DHAMBI HIYO MAUTI, NA HIVYO MAUTI IKAWAFIKIA WATU WOTE KWA SABABU WOTE WAMEFANYA DHAMBI"       

@KWA NINI MWANADAMU ALIKUFA BAADA YA UASI. 

  1. MUNGU ni MTAKATIFU, anatenda anachosema. 
  2. MUNGU ni MWAMINIFU, hulitunza  NENO lake na kulitimiza. 
  3. MUNGU SI MWONGO, alimwambia Mtu siku utakapokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya hakika  UTAKUFA. 
  4. MUNGU HULITUNZA NENO LAKE. 
Note:TO AVOID DEATH is to get rid of sin. 

KWA NINI YESU KRISTO ILIBIDI AFE? 
Kufa kwa YESU ilikuwa ni lazima kwa ajili ya KUMKOMBOA MWANADAMU kutoka kwenye dhambi. 
DHAMBI ilianzisha Mauti kufanya Kazi, ILI dhambi iondolewe Ilihitajika MTU afe kwa ajili ya kuiondoa. YESU KRISTO alishamaliza KAZI hiyo. MSALABANI alitangaza IMEKWISHA! 

@Kwa nini YESU ilibidi afe. 


1.SUBSTITUTION (ALIBEBA GHARAMA YETU), kwa sababu alihitajika mmoja wa kufa kwa ajili ya dhambi yetu). YOHANA 1:29 "Siku yake amwona YESU anakuja kwake, akasema
Tazama, Mwanakondoo wa MUNGU, aichukuaye dhambi ya ULIMWENGU" 

YESU ILI akamilishe Kazi yake, ilibidi auvae MWILI na DAMU ambavyo vilikuwa muhimu katika kukamilisha Kazi yake hapa duniani. MUNGU alihitaji Damu na MWILI kwa sababu DHAMBI husafishwa kwa DAMU. DAMU YA YESU KRISTO imefanyika ondoleo LA dhambi kwa wote WAMWAMINIO. 
@MUNGU ni ROHO, na roho haifi, imeumbiwa umilele, hivyo alihitaji MWILI ili aweze kupitia maisha ya uanadamu na KUTUKOMBOA.

2.TO PAY FOR OUR SIN, WARUMI  6:10 "Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi MARA MOJA TU:
WARUMI 5:8 " BALI MUNGU AONYESHA PENDO LAKE MWENYEWE KWETU SISI, KWA KUWA KRISTO ALIKUFA KWA AJILI YETU, TULIPOKUWA TUNGALI WENYE DHAMBI "
3.DHAMBI YA MWANADAMU ALIOBEBA, ndo ilipelekea KIFO chake. 
4.ILIBIDI AFE, ILI AWEZE KUFUFUKA TENA... ili wote WAMWAMINIO waweze ishi hata baada Ya KIFO. 
5.ALIKUFA, ILI TUHESABIWE TENA HAKI YA KUWA WANA WA MUNGU KATKA UFALME WAKE. 
6 . ALIKUFA ILI KUHARIBU NGUVU YA MAUTI (To put death back to sleep), tangu YESU alipokanyanga ULIMWENGUNI, mauti ilipoteza tena uwezo wa kuua, ndo maana YESU alifufua WAFU na wakawa HAI. 

YOHANA 11 :25 "YESU akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo na uzima. . Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi" 

@Muhimu ndugu msomaji:

  • NI YESU KRISTO pekee aliyekufa kwa ajili ya watu wote, kabila zote, dini zote, Lugha zote na watu WOTE waishio ULIMWENGUNI. 
  • DHAMBI haina tena nguvu tangu YESU alipokanyanga duniani, alibeba dhambi yako, KWA nini unaendelea kuteseka? 
  • NI hasara kubwa na uchaguzi mbaya kufa katika dhambi, WAKATI YESU KRISTO ashamaliza Kazi hiyo miaka mingi iliyopita. 
  • KIFO cha YESU kilikuwa ni lazima, na MUNGU mwenyewe Alikizibitisha (ISAYA 53:1-12). 
  • Ndio maana ni muhimu Ukampa maisha yako BWANA YESU KRISTO. 
  • Unapata tena Uraia wa MBINGUNI na kuingizwa katika UFALME WA MUNGU. 

@KUMBUKA YAFUATAYO :
1.UKIFA KATIKA KRISTO YESU, UNAISHI UZIMA WA MILELE (ETERNAL LIFE) 

2.UKIFA BILA YESU KRISTO, UNAISHI MATESO YA MILELE (ETERNAL DEATH) 
@Unao uwezo wa KUAMUA ni wapi Hatima ya maisha yako,

# LAKINI UKUMBUKE MUNGU BABA MWENYEWE ALIAMUA KUJA KUTUTAFUTA TENA, hivyo sikia sauti yake na URUDI NYUMBANI KWETU MBINGUNI. 

ISAYA 53 :5-6 "
" BALI ALIJERUHIWA KWA MAKOSA YETU, ALICHUBULIWA KWA MAOVU YETU, ADHABU YA AMANI YETU ILI KUWA JUU YAKE, NA KWA KUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA. 6.Sisi kama kondoo tumepotea, Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe, Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.

       WAGALATIA 1:3    "Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa MUNGU BABA, na kwa BWANA wetu YESU KRISTO, ambaye ALIJITOA nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ILI ATUOKOE na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda MUNGU, BABA YETU" 

      Ubarikiwe sana kwa kufuatana nami katika somo hili. 
UTUKUFU Kwa MUNGU BABA, MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO MTAKATIFU aliyewafunulia WANA WAKE siri za UFALME WA MBINGUNI! 
  
Amen. 
075377548
JEMRATH.





Saturday, 11 March 2017

IJUE KWELI YA MUNGU KUHUSU UFALME WA MUNGU ,KANISA LA MUNGU .


 Ninakusalimu katika jina la BWANA WETU YESU KRISTO ALIYE HAI.

Nakukaribisha katika blog hii ambapo utapata kujifunza mengi kuhusu UFALME WA MUNGU,WOKOVU na mengine mengi ya kimasisha.

SOMO:  KANISA LA MUNGU NA HUDUMA ZAKE( JIFUNZE KUHUSU KANISA)

  

A:KANISA LA BWANA YESU KRISTO.
     I.        Maana ya Kanisa.
   II.        Aina za kanisa .
 III.        Chanzo cha kanisa la Agano jipya.
 IV.        Mifano ya kanisa.
   V.        Kazi (HUDUMA ZA KANISA).
 VI.        Nafasi ya ROHO MTAKATIFU katika Kanisa.                                                                                                                                                              VII.        Hitimisho .

1.    MAANA YA KANISA
Maana isiyo ya Kibiblia.
·         Jengo la kanisa mara nyingi watu huita KANISA.-katika agano la kale majengo haya yalitwa;SINAGOGI,HEKALU.
·         Dhehebu au kundi la watu katika dini ya Kikristo.

  Maana ya “KANISA” katika Agano la kale
v  Neno  KANISA ni asili yake limetokana na nene la kiyunani linaloitwa   EKKLESIA
v   Neno –EK likiwa na maana ya “KUTOKA KWA”
v  Neno – KLESIA lina maana ya “KUITWA”
v  Neno  EKKLESIA” likiwa na maana ya –KUITWA KUTOKA KWA.
v  HIVYO neno
 KANISA katika Agano la kale lilimaanisha ;watu ambao wameitwa kutoka kwenye DHAMBI na dunia na ambao wamekusnyika kwa lengo moja.
Maana ya KANISA katika Agano jipya
ü  Waumini wa kwanza katika Agano jipya, walitumia neno kanisa kumaanisha ifuatvyo;


ü  MKUSANYIKO WA WAAMINI NA WAUMINI katika IMANI YA KRISTO.
ü  WARUMI 16:4-15; NISALIMIENI NA KANISA LILILOMO KATIKA NYUMBA YAO.
ü  WAGALATIA 1:2, 1THESALONIKE 1:1.

ü  Ni kundi lote la watu waliozaliwa mara ya pili( UMOJA WA WAKRISTO ULIMWENGUNI KOTE) 1PETRO 1:23. Yakobo 1:18,
ü  Watu walionunuliwa kwa damu ya YESU KRISTO. MATENDO YAMITUME 20:28. UFUNUO 14:4-5.

2.    AINA ZA KANISA
                                                     I.        JENGO
                                                   II.        WATU WA MAHALI PAMOJA
                                                 III.        MTU BINAFSI(MIMI NA WEWE)

3.    CHANZO CHA KANISA LA AGANO JIPYA.
v  MSINGI WA KANISA hili NI YESU KRISTO , BWANA NA MWOKOZI WETU.
v  Kanisa sio shirika la kibinadamu ,kama wengine walivyolifanya.
v  MATHAYO 16:18, “NA JUU YA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA LANGU;WALA MILANGO YA KUZIMU HAITALISHINDA
v  WAEFESO 2:20-22.
v  KANISA LA KRISTO lilizaliwa SIKU YA PENTEKOSTE,ambayo Ahadi ya BABA ya ROHO MTAKATIFU ,ilitimia na MITUME WAKAJAZWA ROHO MTAKATIFU
v  MATENDO 2:1-4, MATENDO 2:41. Watu elfu tatu walipata wokovu siku hiyo, na KANISA likaanzia hapo.

WASHIRIKA  WA KANISA
a)    Mtu anakuwa mshirika wa KANISA la KRISTO mara tu baada ya KUOKOLEWA (MATENDO 2:27)
b)    Watu wengi wamekuwa washirika wa madhehebu mbalimbali ya dini,,bila kuwa WASHIRIKA WA KANISA LA KRISTO.
c)    MTU anapokuwa MKRISTO anahitaji kuungana NA WAUMINI wa KANISA la BWANA ili KUIMARISHA kanisa LA MUNGU.
d)    WASHIRIKI WA KANISA LA KWELI
ü  NI WATAKATIFU-Tumetenganishwa na maisha ya dhambi na tunamwishia MUNGU. WARUMI 1:7
ü  NI NDUGU. WARUMI 8:29
ü  NI WAAMINI.
ü  NI WATEULE.

4.    MIFANO YA KANISA
                                     I.        KANISA NI BIBI –ARUSI NA MWANAKONDOO
v  UFUNUO 21:2
“Nami nikauona mji ule mtakatifu,Yerusalemu  mpya,ukishuka kutoka mbinguni kwa MUNGU,umewekwa tayari,kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe
v  UFUNUO 21:9, MATHAYO 25:6,, YOHANA 3:29. UFUNUO 19:7.
v  BWANA –ARUSI NI YESU KRISTO, KANISA LINAPASWA KUJENGA MSINGI WAKE katika UTAKATIFU.

                                  II.        MASKANI YA MUNGU (HEKALU LA BABA,MWANA NA ROHO MTAKATIFU)
·         YOHANA 14:23    “YESU akajibu,akamwambia,Mtu akinipenda,atalishika neno langu; na BABA  yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya MAKAO kwake
·         YOHANA 14:16-17    “ Nami nitamwomba BABA, naye atawapa Msaidizi mwingine,ili AKAE nanyi hata milele” “bali ninyi mnamtambua ,maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu”
·         1WAKORINTO 6:19-20    AU hamjui ya kuwa mwili wenu ni HEKALU LA ROHO MTAKATIFU aliye ndani yenu,mliyepewa na MUNGU? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; Maana  mlinunuliwa kwa THAMANI. Sasa basi,mtukuzeni MUNGU katika miili yenu.
·         UFUNUO 21:3, 1KORINTO 3:16, 2KORINTO 6:16.
·         KILA mshirika wa KANISA la KRISTO ATAMBUE uthamani huu MKUU tuliopewa na MUNGU,,ili TUWEZE KUKAA katika hali YA UTAKATIFU.

                                III.        MWILI WA KRISTO YESU,MWOKOZI.
Ø  1WAKORINTO 12:24-37.  27  BASI NINYI MMEKUWA MWILI WA KRISTO,NA VIUNGO KILA KIMOJA PEKE YAKE”
Ø  YESU NDIYE BWANA na KIONGOZI MKUU wa kanisa.
Ø  KILA MUUMINI,ni mshirika wa MWILI HUU.
Ø  Wauumini wanahitaji kushirikiana ili waweze kuishi katika MWILI wa KRISTO.
Ø  KILA mwamini ni Mtu na kiungo MUHIMU cha KANISA. Hata kama kinadharauliwa na kuonekana ni cha kawiada bado NI CHA MUHIMU SANA.
Ø  KILA mshirika katika MWILI huu lazima awe na uhusiano wa moja kwa moja na MKUU WA KANISA –YESU KRISTO.
Ø  KANISA NI MWILI WA KIROHO WA YESU kujidhihirisha kwa ULIMWENGU.
Ø  Hivyo washirika,  wote  tunapaswa kuhimizana,kusaidiana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuujenga mwili wa KRISTO.
Ø  WAEFESO 4:16  Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila KIUNGO,kwa kadri ya utendaji wa kila sehemu moja kwa moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika UPENDO

                                 IV.        KANISA NI NGUZO NA MSINGI WA KWELI
1TIMOTHEO 3:15
NI mahali ambapo watu hufundishwa kweli yote ya NENO LA MUNGU.

                                   V.        KANISA NI CHOMBO MILIKIWA NA MUNGU MWENYEWE
TITO 2:14. ,  1 PETRO 2:9
ü  NYUMBA YA ROHO
ü  UKUHANI MTAKATIFU
ü  MAWE YALIYO HAI
ü  MZAO MTEULE
ü  UKUHANI WA KIFALME
ü  TAIFA TAKATIFU
ü  WATU WA MILIKI YA MUNGU.
ü  TAIFA LA MUNGU.

5.    KAZI (HUDUMA YA KANISA LA KRSTO)
MUNGU ,BWANA YESU KRISTO aliweka na kuanzisha KANISA ili kuleta UTUKUFU WA JINA LAKE.
v  Kazi hizi tunaweza kuziangalia katika sehmu tatu ambazo zinamtukuza MUNGU
                                                     i.        KWA NJE’ > INJILI YA YESU KRISTO
                                                    ii.        KWA NDANI’ > TUNAPOJENGANA SISI KWA SISI
                                                  iii.        ‘KWA JUU’ >KATIKA IBADA


KAZI ZA KANISA
A.     Kuhubiri injili kwa  kila kiumbe ulimwenguni kote( HABARI NJEMA ZA UFALME WAMUNGU)
MARKO 16:15, MATHAYO 28:19-20.   1PETRO 2:9,MATENDO 1:8.
B.   Kujengana Nafsi (mwili wa KRISTO)  1KORINTO 14:26.
C.   HUMFANYIA MUNGU IBADA . WEABRANIA 13:15, 10:25.  NJIA ambazo tunamwabudu MUNGU
v  Kukusanyika pamoja, mathayo 18:20,,ebrania 10:25.
v  Kupitia mziki na nyimbo. Waefeso 5:19,, zaburi 50:23,ZABURI 150
v  Kwa njia ya MAOMBI        .MATENDO 2:46-47,4:24. MARKO 11:17
v  KUTOA
v  Kwa NJIA YA ROHO MTAKATIFU
v  KUHIDHABIHU NMIILI YETU, WARUMI 12:1-2.
D.KANISA HUMRUSU ROHO MTAKATIFU katika HUDUMA ZOTE. 1KORINTO 12:4
E.HUFUNDISHA KWELI YA NENO LA MUNGU.kupitia vipindi mbalimbali,Sunday school,vijana.
F.HUBATIZA KWA MAJI MENGI. MATHAYO 28:19
G.HUKUMBUKA KIFO CHA BWANA kwa njia ya MEZA YA BWANA. LUKA 22:20.
H. HUFANYA USHIRIKA MBALIMBALI, kuomba kwa pamoja, kula kwa pamoja na kushirikiana.
I.kanisa HUSHEREKEA, mfano;ndoa,watoto kuombewa,vifo, Christmas,pasaka,siku  ya BWANA
J.KANISA HUKUA
K.HUHUDUMIA WATU; KUSAIDIA wahitaji,waliopotea,na kuwalea waumini wapya.
PIA kazi nyingine muhimu ni pamoja na
v  KUMTII KRISTO kwa kuwatii wnadamu. WAEBRANIA 13:17, TITO 3:1-2. 1THESALONIKE 5:12, MALAKI 2:7.
v  KUITEGEMEZA NYUMBA YA MUNGU
v  KUIJENGA NYUMBA YA KUABUDIA
v  KUITEGEMEZA NYUMBA YA MCHUNGAJI
v  1WAKORINTO 9:7-11; MATHAYO 25;31-46;
v  KUTOA ZAKA   MALAKI 3:10-12., MITHALI 10:27. MITHALI 3:9-10.


6.    NAFASI YA ROHO MTAKATIFU KATIKA KANISA LA LEO. ROHO wa MUNGU ndio chanzo cha KANISA LA KWANZA ,hivyo basi tunapaswa kutambua na kumpa nafasi ya PEKEE na ya  KWANZA katika MAISHA YETU na HUDUMA katiKA kanisa lake.
ü  Wagalatia 4:6, waefeso 4:4
ü  YEYE ndiye kiongozi,mwalimu wetu  hivyo ni vyema katika maamuzi yote tuyafanyayo KUMSHRIKISHA ili tuweze kukua KATIKA IMANI YA YESU KRISTO.
ü  KANISA ,tunapaswa kusisitiza kila mmoja wetu, kuhusu KUJAZWA NA kutembea,kuishi katika ROHO MTAKATIFU

7.    HITIMISHO
“KANISA ni MWILI HALISI WA KIROHO WA YESU KRISTO, hivyo tunapaswa kuwa na kutmbea na kuishi katika UTAKATIFU
v  LUKA 18: 7-8  NA MUNGU,JE! HATAWAPATIA HAKI WATEULE WAKE WANAOMLILIA MCHANA NA USIKU, NAYE NI MVUMILIVU KWAO?8 NAWAAMBIA,ATAWAPATIA HAKI UPESI; WALAKINI, ATAKAPOKUJA MWANA WA ADAMU, JE!ATAIONA IMANI DUNIANI?
HESHIMA NA UTUKUFU KWAKO BWANA NA MWOKOZI WETU YESU KRISTO UNAYE TUWEZESHA! Barikiwa sana wote.By jbrev.