Friday, 24 March 2017

IBADA YA KWELI MBELE ZA MUNGU BABA.

 Nawasalimu katika jina la MUNGU  BABA, MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO MTAKATIFU.
 Karibuni tena tuendelee kujifunza habari za UFALME WA MUNGU. 

SOMO :IBADA YA KWELI MBELE ZA MUNGU. 
  
  Utangulizi, NENO KUABUDU linaoneka kwa mara ya kwanza katika MWANZO 22 :5 "Ibrahimu akawambia vijana wake, kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, TUKAABUDU, na kuwarudia tena" 

MAANA YA IBADA ni hali ya Moyo wa mwanadamu kuwa na USHIRIKA NA MUNGU. 
MOYO wa mwanadamu umeumbiwa na una Hulka ya KUFANYA IBADA. Pia kusudi la Mungu kumwumba mwanadamu ni ILI awe na USHIRIKA naye. 

Yohana 4:23 - 24 "Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabudio halisi wstamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 
Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli" 

    IBADA YA KWELI HUHUSISHA :
  1. MUNGU. 
  2. MWANADAMU. 
  3. MADHABAHU (MOYO), 1Falme 18 :30. 
  4. ROHO MTAKATIFU. MATHAYO 18:19-20 
  5. UTAKATIFU. 
  MADHABAHU YA KWELI NI MOYO WAKO - mahali ambapo MUNGU na mtu hukutana. 
Mwanadamu, baada Ya kuokoka, ROHO MTAKATIFU anaingia ndani ya mtu na kuanza Kuishi naye. 
Hivyo, MTU hufanyika kuwa HEKALU LA MUNGU.
  •  1 wakorinto 6:19 - 20 
  • Rumi 12:1 
@Madhabahu (MOYO wako) inatakiwa kuwa 
  • NI mahali pa dhabihu (kujitoa mbele za MUNGU) 
  • Ni mahali pa kujikana (kuacha vitu vyote, shughuli zote, unavyovipenda, n.k. (UNAKUBALI NA KUMPA MUNGU NAFASI  YA KWANZA maishani mwako) 
  • Ni mahali pa moto (sehemu inahitajiwa kutunzwa siku zote na mda wote. MITHALI 4':23 "Linda Moyo wako kuliko yote uyalindayo, Maana ndiko zitokako  chemchemi za uzima" 
  • Ni mahali pa kiu na njaa ya HAKI ya kukutana na MUNGU. 
UMUHIMU WA KUWA NA IBADA MAISHANI MWAKO. 
@UNAKUWA MALI YA MUNGU 
@UNAKUWA NA USALAMA 
@UPENDO WA MUNGU UZALIWA NA KUACHILIWA MAISHANI MWAKO. 
UTAFANYIKA BARAKA KWA WATU, JAMII NA TAIFA KWA UJUMLA. 

MAMBO YA MUHIMU NA KUKUMBUKA ZAIDI. 
  1. Madhabahu (MOYO) ni sehemu muhimu katika maisha ya IBADA. 
  2. MADHABAHU (MOYO) ni sehemu muhimu katika USHIRIKA NA MUNGU. 
  3. NI wajibu wa mtu kuandaa madhabahu yake katika MAISHA ya IBADA. 
  4. MADHABAHU ni sehemu inayopaswa kutoa Harufu nzuri, safi na ya KUMPENDEZA BWANA. 
  5. Madhabahu lazima itunzwe siku zote (MAOMBI, NENO) 
  6. MADHABAHU isipotunzwa, mtu hatafurahia uzuri wa IBADA. 
  7. MOYO UKIWA HAI KWENYE MAISHA kYA IBADA NA MUNGU, UNATENGENEZA MAISHA NA HATIMA ILIYO HAI. 
  8. ROHO MTAKATIFU ni mtu muhimu sana katika maisha ya IBADA (hutuongoza, hutufariji, hutufundisha neno, hutupa siri za MUNGU, hututia nguvu) 
  9. Ni wajibu wa mtu, kutambua UMUHIMU WA ROHO MTAKATIFU, na kumshirikisha katika maisha yetu ya kila siku. 
  10. IBADA YA KWELI NA YA PEKEE NI KUMWABUDU MUUMBA WETU ALIYETUUMBA. 

   Pia, ibada huambatana na SIFA, NYIMBO, TENZI, KUSUJUDU, SADAKA, NENO. 
"
         "HAZINA YAKO ILIPO, NDIPO NA MOYO WAKO UTAKAPOKUWA 
 MUNGU BABA WA MBINGUNI awabarki sana, karibuni tena. 

4 comments:

  1. Nifanye nini ili niweze kuabudu katika kweli na roho? Na nifanye nini ili niweze kumpokea Roho Mtakatifu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kuacha...na uishi maisha matakatifu..
      Jifunze kuhusu Roho mtakatifu na anza kuomba Mungu akujaze Roho wake mtakatifu...maana ni ahadi yake

      Delete