Wednesday, 15 March 2017

FAHAMU UNDANI WA KWA NINI YESU ILIBIDI AJE NA KUFA ILI KUTUOKOA.

Rafiki, ndugu na mpendwa, nakusalimu katika JINA LA MUNGU BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU.
   Napenda kukukaribisha katika somo hili, ili Tuweze kujifunza ZAIDI kuhusu UFALME WA MUNGU.

SOMO : KWA NINI YESU ILIBIDI AJE NA KUFA MSALABANI ILI KUTUOKOA MIMI NA WEWE? 
   
YESU KRISTO ni mtu aliyewahi Kuishi hapa duniani, na kuacha HISTORIA mpaka leo, kutokea miaka 2000 iliyopita. Ni mtu Pekee ambaye jina lake, kazi zake na ujumbe wake vinatajwa hata leo kuliko mtu mwingine aliyewahi Kuishi hapa duniani. 

VITU AMBAVYO BADO VINATAJWA KUHUSU YESU KRISTO LEO. 

  1. KUZALIWA KWAKE, alivyozaliwa kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU kupitia Mariamu Bikira.
  2. MAISHA YA YESU, Maisha bila dhambi, miujiza yake. 
  3. UJUMBE WA YESU KUHUSU UFALME WA MUNGU, alitangaza msamaha wa dhambi, uzima wa MILELE. Upendo WA MUNGU BABA. 
  4. KIFO CHA YESU, jinsi alivyokufa, kwa nini alikufa, nani alimuua. 
  5. KUZIKWA KWAKE (KABURI ALILOZIKWA) 
  6. KUFUFUKA KWA YESU KRISTO, jinsi alivyofufuka na kwa nini ilibidi afufuke. 
  7. KURUDI KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI, ni wakati gani atarudi na kwa nini.
   Hivyo ni baadhi ya vitu vinavyoleta maswali kwa wengi, KUHUSU YESU KRISTO MWOKOZI. Watu wengi wakiwemo wasomi, wanasayansi, wanafilosofi, atheists, religious people, wamebaki bila majibu kuhusu HUYU YESU KRISTO, Wengine wakisema alikuwa mtu wa kawaida, mtu mwema,n.k. WAKIKATAA UKWELI ULIO WAZI. 

 TUANGALIE SASA KWA NINI YESU KRISTO, DUNIANI.
Tuangalie vipengele vifutavyo kwanza kabla ya kwenda ndani ZAIDI, tujue mwanzo wa YOTE haya!

KUUMBWA KWA MWANADAMU, Mwanzo 1:27 "MUNGU AKAUMBA MTU KWA MFANO   WAKE, KWA MFANO WA MUNGU ALIMWUMBA, MWANAMME NA MWANAMKE ALIWAUMBA"    Mwanzo 2:7, MUNGU alituumba kwa mfano wake, lengo lake tuweze kumwakilisha katika ULIMWENGU ili kuutunza UTUKUFU wake, MUNGU alupoumba vitu vyote aliviumba kwa UTUKUFU WAKE.                                                        ASILI yetu tokea Mwanzo ni MBINGUNI, UASI ulifanya tupoteze asili yetu ya MBINGUNI.  MUNGU alipoumba vitu na mwanadamu, alimpa mwanadamu MAMLAKA ya KUVITAWALA na kuvitunza, hiyo yote MUNGU, lengo lake ni kutushirikisha UTUKUFU wake katika UFALME WA MUNGU. 

2.CHANZO CHA KIFO(MAUTI) , DHAMBI.  MWANZO 2:16-17 "BWANA MUNGU akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mtu wa bustani waweza kula, Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo UTAKUFA HAKIKA"
  •   AGIZO LA MUNGU kwa MTU linahusisha vitu vitatu muhimu :1 . MTU 2.MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA 3.KIFO (UTAKUFA(MAUTI ). Fahamu yafautayo ni muhimu :
  • MUNGU aliumba KIFO. (MAUTI) 
  • KIFO kilikuwepo hata kabla hakijaanza kuua. 
  • KIFO kiliumbwa kikiwa hakina nguvu ya kuua (kiliumbwa kikiwa hakifanyi Kazi) 
  • KIFO kiliumbwa kikiwa hakina UHAI. 
  • Mauti iliumbwa bila tatizo (Normal). 
  • MUNGU alimwambia MTU siku utakapokula Tunda LA Mti wa ujuzi wa mema na mabaya, UTAKUFA, MTU alikuwa na uwezo wa kuchagua KIFO au kuendelea KUISHI katika BUSTANI YA EDENI. 

  • KUMBUKUMBU LA TORATI 30:19-20 "Nazishuhudiza mbingu na nchi hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako UZIMA NA MAUTI, baraka na laana, BASI chagau UZIMA ili uwe hai, wewe na uzao wako, KUMPENDA BWANA, MUNGU, WAKO, KUITII SAUTI YAKE, NA KUSHIKAMANA NAYE, KWANI HIYO NDIYO UZIMA WAKO, NA WINGI WA SIKU ZAKO, UPATE KUKAA KATIKA nchi BWANA aliyaowaapia baba zako, Ibrahim na Isaka na Yakobo, kuwa atawapa "
DHAMBI NA KIFO BAADA YA UASI. 
           DHAMBI ni uasi dhidi ya amri ya  MUNGU (REBELLION AGAINST THE WILL OF GOD) or TO MISS OUT the PRESENCE OF GOD. 

Dhambi ya mtu katika bustani ya Edeni ilikipa KIFO uwezo wa kufanya Kazi na kuanza Kuua tangu wakati huo, KIFO ni matokeo ya dhambi, kutotii amri ya Mungu (DISOBEDIENCE OF GOD'S WORD). 
Baada Ya dhambi Mauti ikawa na tatizo (abnormal) ikaanza kuua. 

Dhambi ya ADAMU, ikakipa ruhusa KIFO kuua.

NINI MAANA YA KIFO (MAUTI)
1.Kuondoka kwa ROHO MTAKATIFU katika maisha ya mtu (Very dangerous) (departure of HOLY SPIRIT, leaving man spirit) 
2.KUTOKA KATIKA UWEPO WA MUNGU (departure of Man in presence of GOD) 
3.Kuondoka kwa Roho ya mtu (departure of Man spirit, leaving human being). 

Note :Tangu siku ile mtu alipokula matunda, alipoasi Amri ya MUNGU, alikufa siku hiyo , japo aliendelea Kuishi kwa maisha ya nje, Na Vizazi vyote vilivyofuatia vilizaliwa katika dhambi hiyo. 
Pia, MUNGU hakumuua Adamu BALI KIFO (MAUTI) kilimuua Adamu. 

WARUMI 5:12 "KWA HIYO, KAMA KWA MTU MMOJA DHAMBI ILIINGIA ULIMWENGUNI, NA KWA DHAMBI HIYO MAUTI, NA HIVYO MAUTI IKAWAFIKIA WATU WOTE KWA SABABU WOTE WAMEFANYA DHAMBI"       

@KWA NINI MWANADAMU ALIKUFA BAADA YA UASI. 

  1. MUNGU ni MTAKATIFU, anatenda anachosema. 
  2. MUNGU ni MWAMINIFU, hulitunza  NENO lake na kulitimiza. 
  3. MUNGU SI MWONGO, alimwambia Mtu siku utakapokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya hakika  UTAKUFA. 
  4. MUNGU HULITUNZA NENO LAKE. 
Note:TO AVOID DEATH is to get rid of sin. 

KWA NINI YESU KRISTO ILIBIDI AFE? 
Kufa kwa YESU ilikuwa ni lazima kwa ajili ya KUMKOMBOA MWANADAMU kutoka kwenye dhambi. 
DHAMBI ilianzisha Mauti kufanya Kazi, ILI dhambi iondolewe Ilihitajika MTU afe kwa ajili ya kuiondoa. YESU KRISTO alishamaliza KAZI hiyo. MSALABANI alitangaza IMEKWISHA! 

@Kwa nini YESU ilibidi afe. 


1.SUBSTITUTION (ALIBEBA GHARAMA YETU), kwa sababu alihitajika mmoja wa kufa kwa ajili ya dhambi yetu). YOHANA 1:29 "Siku yake amwona YESU anakuja kwake, akasema
Tazama, Mwanakondoo wa MUNGU, aichukuaye dhambi ya ULIMWENGU" 

YESU ILI akamilishe Kazi yake, ilibidi auvae MWILI na DAMU ambavyo vilikuwa muhimu katika kukamilisha Kazi yake hapa duniani. MUNGU alihitaji Damu na MWILI kwa sababu DHAMBI husafishwa kwa DAMU. DAMU YA YESU KRISTO imefanyika ondoleo LA dhambi kwa wote WAMWAMINIO. 
@MUNGU ni ROHO, na roho haifi, imeumbiwa umilele, hivyo alihitaji MWILI ili aweze kupitia maisha ya uanadamu na KUTUKOMBOA.

2.TO PAY FOR OUR SIN, WARUMI  6:10 "Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi MARA MOJA TU:
WARUMI 5:8 " BALI MUNGU AONYESHA PENDO LAKE MWENYEWE KWETU SISI, KWA KUWA KRISTO ALIKUFA KWA AJILI YETU, TULIPOKUWA TUNGALI WENYE DHAMBI "
3.DHAMBI YA MWANADAMU ALIOBEBA, ndo ilipelekea KIFO chake. 
4.ILIBIDI AFE, ILI AWEZE KUFUFUKA TENA... ili wote WAMWAMINIO waweze ishi hata baada Ya KIFO. 
5.ALIKUFA, ILI TUHESABIWE TENA HAKI YA KUWA WANA WA MUNGU KATKA UFALME WAKE. 
6 . ALIKUFA ILI KUHARIBU NGUVU YA MAUTI (To put death back to sleep), tangu YESU alipokanyanga ULIMWENGUNI, mauti ilipoteza tena uwezo wa kuua, ndo maana YESU alifufua WAFU na wakawa HAI. 

YOHANA 11 :25 "YESU akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo na uzima. . Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi" 

@Muhimu ndugu msomaji:

  • NI YESU KRISTO pekee aliyekufa kwa ajili ya watu wote, kabila zote, dini zote, Lugha zote na watu WOTE waishio ULIMWENGUNI. 
  • DHAMBI haina tena nguvu tangu YESU alipokanyanga duniani, alibeba dhambi yako, KWA nini unaendelea kuteseka? 
  • NI hasara kubwa na uchaguzi mbaya kufa katika dhambi, WAKATI YESU KRISTO ashamaliza Kazi hiyo miaka mingi iliyopita. 
  • KIFO cha YESU kilikuwa ni lazima, na MUNGU mwenyewe Alikizibitisha (ISAYA 53:1-12). 
  • Ndio maana ni muhimu Ukampa maisha yako BWANA YESU KRISTO. 
  • Unapata tena Uraia wa MBINGUNI na kuingizwa katika UFALME WA MUNGU. 

@KUMBUKA YAFUATAYO :
1.UKIFA KATIKA KRISTO YESU, UNAISHI UZIMA WA MILELE (ETERNAL LIFE) 

2.UKIFA BILA YESU KRISTO, UNAISHI MATESO YA MILELE (ETERNAL DEATH) 
@Unao uwezo wa KUAMUA ni wapi Hatima ya maisha yako,

# LAKINI UKUMBUKE MUNGU BABA MWENYEWE ALIAMUA KUJA KUTUTAFUTA TENA, hivyo sikia sauti yake na URUDI NYUMBANI KWETU MBINGUNI. 

ISAYA 53 :5-6 "
" BALI ALIJERUHIWA KWA MAKOSA YETU, ALICHUBULIWA KWA MAOVU YETU, ADHABU YA AMANI YETU ILI KUWA JUU YAKE, NA KWA KUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA. 6.Sisi kama kondoo tumepotea, Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe, Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.

       WAGALATIA 1:3    "Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa MUNGU BABA, na kwa BWANA wetu YESU KRISTO, ambaye ALIJITOA nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ILI ATUOKOE na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda MUNGU, BABA YETU" 

      Ubarikiwe sana kwa kufuatana nami katika somo hili. 
UTUKUFU Kwa MUNGU BABA, MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO MTAKATIFU aliyewafunulia WANA WAKE siri za UFALME WA MBINGUNI! 
  
Amen. 
075377548
JEMRATH.





2 comments:

  1. Mbarikiwe mno nmepata kitu kikubwa sana sana

    ReplyDelete
  2. Asante sana kwa Somo hili. Ubarikiwe. Cha kufanya ni kutubu dhambi na kuziacha Ili mtu aweze kupata uzima wa Milele. Mith. 28:13

    ReplyDelete