Friday, 24 March 2017

IBADA YA KWELI MBELE ZA MUNGU BABA.

 Nawasalimu katika jina la MUNGU  BABA, MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO MTAKATIFU.
 Karibuni tena tuendelee kujifunza habari za UFALME WA MUNGU. 

SOMO :IBADA YA KWELI MBELE ZA MUNGU. 
  
  Utangulizi, NENO KUABUDU linaoneka kwa mara ya kwanza katika MWANZO 22 :5 "Ibrahimu akawambia vijana wake, kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, TUKAABUDU, na kuwarudia tena" 

MAANA YA IBADA ni hali ya Moyo wa mwanadamu kuwa na USHIRIKA NA MUNGU. 
MOYO wa mwanadamu umeumbiwa na una Hulka ya KUFANYA IBADA. Pia kusudi la Mungu kumwumba mwanadamu ni ILI awe na USHIRIKA naye. 

Yohana 4:23 - 24 "Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabudio halisi wstamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 
Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli" 

    IBADA YA KWELI HUHUSISHA :
  1. MUNGU. 
  2. MWANADAMU. 
  3. MADHABAHU (MOYO), 1Falme 18 :30. 
  4. ROHO MTAKATIFU. MATHAYO 18:19-20 
  5. UTAKATIFU. 
  MADHABAHU YA KWELI NI MOYO WAKO - mahali ambapo MUNGU na mtu hukutana. 
Mwanadamu, baada Ya kuokoka, ROHO MTAKATIFU anaingia ndani ya mtu na kuanza Kuishi naye. 
Hivyo, MTU hufanyika kuwa HEKALU LA MUNGU.
  •  1 wakorinto 6:19 - 20 
  • Rumi 12:1 
@Madhabahu (MOYO wako) inatakiwa kuwa 
  • NI mahali pa dhabihu (kujitoa mbele za MUNGU) 
  • Ni mahali pa kujikana (kuacha vitu vyote, shughuli zote, unavyovipenda, n.k. (UNAKUBALI NA KUMPA MUNGU NAFASI  YA KWANZA maishani mwako) 
  • Ni mahali pa moto (sehemu inahitajiwa kutunzwa siku zote na mda wote. MITHALI 4':23 "Linda Moyo wako kuliko yote uyalindayo, Maana ndiko zitokako  chemchemi za uzima" 
  • Ni mahali pa kiu na njaa ya HAKI ya kukutana na MUNGU. 
UMUHIMU WA KUWA NA IBADA MAISHANI MWAKO. 
@UNAKUWA MALI YA MUNGU 
@UNAKUWA NA USALAMA 
@UPENDO WA MUNGU UZALIWA NA KUACHILIWA MAISHANI MWAKO. 
UTAFANYIKA BARAKA KWA WATU, JAMII NA TAIFA KWA UJUMLA. 

MAMBO YA MUHIMU NA KUKUMBUKA ZAIDI. 
  1. Madhabahu (MOYO) ni sehemu muhimu katika maisha ya IBADA. 
  2. MADHABAHU (MOYO) ni sehemu muhimu katika USHIRIKA NA MUNGU. 
  3. NI wajibu wa mtu kuandaa madhabahu yake katika MAISHA ya IBADA. 
  4. MADHABAHU ni sehemu inayopaswa kutoa Harufu nzuri, safi na ya KUMPENDEZA BWANA. 
  5. Madhabahu lazima itunzwe siku zote (MAOMBI, NENO) 
  6. MADHABAHU isipotunzwa, mtu hatafurahia uzuri wa IBADA. 
  7. MOYO UKIWA HAI KWENYE MAISHA kYA IBADA NA MUNGU, UNATENGENEZA MAISHA NA HATIMA ILIYO HAI. 
  8. ROHO MTAKATIFU ni mtu muhimu sana katika maisha ya IBADA (hutuongoza, hutufariji, hutufundisha neno, hutupa siri za MUNGU, hututia nguvu) 
  9. Ni wajibu wa mtu, kutambua UMUHIMU WA ROHO MTAKATIFU, na kumshirikisha katika maisha yetu ya kila siku. 
  10. IBADA YA KWELI NA YA PEKEE NI KUMWABUDU MUUMBA WETU ALIYETUUMBA. 

   Pia, ibada huambatana na SIFA, NYIMBO, TENZI, KUSUJUDU, SADAKA, NENO. 
"
         "HAZINA YAKO ILIPO, NDIPO NA MOYO WAKO UTAKAPOKUWA 
 MUNGU BABA WA MBINGUNI awabarki sana, karibuni tena. 

Wednesday, 15 March 2017

FAHAMU UNDANI WA KWA NINI YESU ILIBIDI AJE NA KUFA ILI KUTUOKOA.

Rafiki, ndugu na mpendwa, nakusalimu katika JINA LA MUNGU BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU.
   Napenda kukukaribisha katika somo hili, ili Tuweze kujifunza ZAIDI kuhusu UFALME WA MUNGU.

SOMO : KWA NINI YESU ILIBIDI AJE NA KUFA MSALABANI ILI KUTUOKOA MIMI NA WEWE? 
   
YESU KRISTO ni mtu aliyewahi Kuishi hapa duniani, na kuacha HISTORIA mpaka leo, kutokea miaka 2000 iliyopita. Ni mtu Pekee ambaye jina lake, kazi zake na ujumbe wake vinatajwa hata leo kuliko mtu mwingine aliyewahi Kuishi hapa duniani. 

VITU AMBAVYO BADO VINATAJWA KUHUSU YESU KRISTO LEO. 

  1. KUZALIWA KWAKE, alivyozaliwa kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU kupitia Mariamu Bikira.
  2. MAISHA YA YESU, Maisha bila dhambi, miujiza yake. 
  3. UJUMBE WA YESU KUHUSU UFALME WA MUNGU, alitangaza msamaha wa dhambi, uzima wa MILELE. Upendo WA MUNGU BABA. 
  4. KIFO CHA YESU, jinsi alivyokufa, kwa nini alikufa, nani alimuua. 
  5. KUZIKWA KWAKE (KABURI ALILOZIKWA) 
  6. KUFUFUKA KWA YESU KRISTO, jinsi alivyofufuka na kwa nini ilibidi afufuke. 
  7. KURUDI KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI, ni wakati gani atarudi na kwa nini.
   Hivyo ni baadhi ya vitu vinavyoleta maswali kwa wengi, KUHUSU YESU KRISTO MWOKOZI. Watu wengi wakiwemo wasomi, wanasayansi, wanafilosofi, atheists, religious people, wamebaki bila majibu kuhusu HUYU YESU KRISTO, Wengine wakisema alikuwa mtu wa kawaida, mtu mwema,n.k. WAKIKATAA UKWELI ULIO WAZI. 

 TUANGALIE SASA KWA NINI YESU KRISTO, DUNIANI.
Tuangalie vipengele vifutavyo kwanza kabla ya kwenda ndani ZAIDI, tujue mwanzo wa YOTE haya!

KUUMBWA KWA MWANADAMU, Mwanzo 1:27 "MUNGU AKAUMBA MTU KWA MFANO   WAKE, KWA MFANO WA MUNGU ALIMWUMBA, MWANAMME NA MWANAMKE ALIWAUMBA"    Mwanzo 2:7, MUNGU alituumba kwa mfano wake, lengo lake tuweze kumwakilisha katika ULIMWENGU ili kuutunza UTUKUFU wake, MUNGU alupoumba vitu vyote aliviumba kwa UTUKUFU WAKE.                                                        ASILI yetu tokea Mwanzo ni MBINGUNI, UASI ulifanya tupoteze asili yetu ya MBINGUNI.  MUNGU alipoumba vitu na mwanadamu, alimpa mwanadamu MAMLAKA ya KUVITAWALA na kuvitunza, hiyo yote MUNGU, lengo lake ni kutushirikisha UTUKUFU wake katika UFALME WA MUNGU. 

2.CHANZO CHA KIFO(MAUTI) , DHAMBI.  MWANZO 2:16-17 "BWANA MUNGU akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mtu wa bustani waweza kula, Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo UTAKUFA HAKIKA"
  •   AGIZO LA MUNGU kwa MTU linahusisha vitu vitatu muhimu :1 . MTU 2.MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA 3.KIFO (UTAKUFA(MAUTI ). Fahamu yafautayo ni muhimu :
  • MUNGU aliumba KIFO. (MAUTI) 
  • KIFO kilikuwepo hata kabla hakijaanza kuua. 
  • KIFO kiliumbwa kikiwa hakina nguvu ya kuua (kiliumbwa kikiwa hakifanyi Kazi) 
  • KIFO kiliumbwa kikiwa hakina UHAI. 
  • Mauti iliumbwa bila tatizo (Normal). 
  • MUNGU alimwambia MTU siku utakapokula Tunda LA Mti wa ujuzi wa mema na mabaya, UTAKUFA, MTU alikuwa na uwezo wa kuchagua KIFO au kuendelea KUISHI katika BUSTANI YA EDENI. 

  • KUMBUKUMBU LA TORATI 30:19-20 "Nazishuhudiza mbingu na nchi hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako UZIMA NA MAUTI, baraka na laana, BASI chagau UZIMA ili uwe hai, wewe na uzao wako, KUMPENDA BWANA, MUNGU, WAKO, KUITII SAUTI YAKE, NA KUSHIKAMANA NAYE, KWANI HIYO NDIYO UZIMA WAKO, NA WINGI WA SIKU ZAKO, UPATE KUKAA KATIKA nchi BWANA aliyaowaapia baba zako, Ibrahim na Isaka na Yakobo, kuwa atawapa "
DHAMBI NA KIFO BAADA YA UASI. 
           DHAMBI ni uasi dhidi ya amri ya  MUNGU (REBELLION AGAINST THE WILL OF GOD) or TO MISS OUT the PRESENCE OF GOD. 

Dhambi ya mtu katika bustani ya Edeni ilikipa KIFO uwezo wa kufanya Kazi na kuanza Kuua tangu wakati huo, KIFO ni matokeo ya dhambi, kutotii amri ya Mungu (DISOBEDIENCE OF GOD'S WORD). 
Baada Ya dhambi Mauti ikawa na tatizo (abnormal) ikaanza kuua. 

Dhambi ya ADAMU, ikakipa ruhusa KIFO kuua.

NINI MAANA YA KIFO (MAUTI)
1.Kuondoka kwa ROHO MTAKATIFU katika maisha ya mtu (Very dangerous) (departure of HOLY SPIRIT, leaving man spirit) 
2.KUTOKA KATIKA UWEPO WA MUNGU (departure of Man in presence of GOD) 
3.Kuondoka kwa Roho ya mtu (departure of Man spirit, leaving human being). 

Note :Tangu siku ile mtu alipokula matunda, alipoasi Amri ya MUNGU, alikufa siku hiyo , japo aliendelea Kuishi kwa maisha ya nje, Na Vizazi vyote vilivyofuatia vilizaliwa katika dhambi hiyo. 
Pia, MUNGU hakumuua Adamu BALI KIFO (MAUTI) kilimuua Adamu. 

WARUMI 5:12 "KWA HIYO, KAMA KWA MTU MMOJA DHAMBI ILIINGIA ULIMWENGUNI, NA KWA DHAMBI HIYO MAUTI, NA HIVYO MAUTI IKAWAFIKIA WATU WOTE KWA SABABU WOTE WAMEFANYA DHAMBI"       

@KWA NINI MWANADAMU ALIKUFA BAADA YA UASI. 

  1. MUNGU ni MTAKATIFU, anatenda anachosema. 
  2. MUNGU ni MWAMINIFU, hulitunza  NENO lake na kulitimiza. 
  3. MUNGU SI MWONGO, alimwambia Mtu siku utakapokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya hakika  UTAKUFA. 
  4. MUNGU HULITUNZA NENO LAKE. 
Note:TO AVOID DEATH is to get rid of sin. 

KWA NINI YESU KRISTO ILIBIDI AFE? 
Kufa kwa YESU ilikuwa ni lazima kwa ajili ya KUMKOMBOA MWANADAMU kutoka kwenye dhambi. 
DHAMBI ilianzisha Mauti kufanya Kazi, ILI dhambi iondolewe Ilihitajika MTU afe kwa ajili ya kuiondoa. YESU KRISTO alishamaliza KAZI hiyo. MSALABANI alitangaza IMEKWISHA! 

@Kwa nini YESU ilibidi afe. 


1.SUBSTITUTION (ALIBEBA GHARAMA YETU), kwa sababu alihitajika mmoja wa kufa kwa ajili ya dhambi yetu). YOHANA 1:29 "Siku yake amwona YESU anakuja kwake, akasema
Tazama, Mwanakondoo wa MUNGU, aichukuaye dhambi ya ULIMWENGU" 

YESU ILI akamilishe Kazi yake, ilibidi auvae MWILI na DAMU ambavyo vilikuwa muhimu katika kukamilisha Kazi yake hapa duniani. MUNGU alihitaji Damu na MWILI kwa sababu DHAMBI husafishwa kwa DAMU. DAMU YA YESU KRISTO imefanyika ondoleo LA dhambi kwa wote WAMWAMINIO. 
@MUNGU ni ROHO, na roho haifi, imeumbiwa umilele, hivyo alihitaji MWILI ili aweze kupitia maisha ya uanadamu na KUTUKOMBOA.

2.TO PAY FOR OUR SIN, WARUMI  6:10 "Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi MARA MOJA TU:
WARUMI 5:8 " BALI MUNGU AONYESHA PENDO LAKE MWENYEWE KWETU SISI, KWA KUWA KRISTO ALIKUFA KWA AJILI YETU, TULIPOKUWA TUNGALI WENYE DHAMBI "
3.DHAMBI YA MWANADAMU ALIOBEBA, ndo ilipelekea KIFO chake. 
4.ILIBIDI AFE, ILI AWEZE KUFUFUKA TENA... ili wote WAMWAMINIO waweze ishi hata baada Ya KIFO. 
5.ALIKUFA, ILI TUHESABIWE TENA HAKI YA KUWA WANA WA MUNGU KATKA UFALME WAKE. 
6 . ALIKUFA ILI KUHARIBU NGUVU YA MAUTI (To put death back to sleep), tangu YESU alipokanyanga ULIMWENGUNI, mauti ilipoteza tena uwezo wa kuua, ndo maana YESU alifufua WAFU na wakawa HAI. 

YOHANA 11 :25 "YESU akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo na uzima. . Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi" 

@Muhimu ndugu msomaji:

  • NI YESU KRISTO pekee aliyekufa kwa ajili ya watu wote, kabila zote, dini zote, Lugha zote na watu WOTE waishio ULIMWENGUNI. 
  • DHAMBI haina tena nguvu tangu YESU alipokanyanga duniani, alibeba dhambi yako, KWA nini unaendelea kuteseka? 
  • NI hasara kubwa na uchaguzi mbaya kufa katika dhambi, WAKATI YESU KRISTO ashamaliza Kazi hiyo miaka mingi iliyopita. 
  • KIFO cha YESU kilikuwa ni lazima, na MUNGU mwenyewe Alikizibitisha (ISAYA 53:1-12). 
  • Ndio maana ni muhimu Ukampa maisha yako BWANA YESU KRISTO. 
  • Unapata tena Uraia wa MBINGUNI na kuingizwa katika UFALME WA MUNGU. 

@KUMBUKA YAFUATAYO :
1.UKIFA KATIKA KRISTO YESU, UNAISHI UZIMA WA MILELE (ETERNAL LIFE) 

2.UKIFA BILA YESU KRISTO, UNAISHI MATESO YA MILELE (ETERNAL DEATH) 
@Unao uwezo wa KUAMUA ni wapi Hatima ya maisha yako,

# LAKINI UKUMBUKE MUNGU BABA MWENYEWE ALIAMUA KUJA KUTUTAFUTA TENA, hivyo sikia sauti yake na URUDI NYUMBANI KWETU MBINGUNI. 

ISAYA 53 :5-6 "
" BALI ALIJERUHIWA KWA MAKOSA YETU, ALICHUBULIWA KWA MAOVU YETU, ADHABU YA AMANI YETU ILI KUWA JUU YAKE, NA KWA KUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA. 6.Sisi kama kondoo tumepotea, Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe, Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.

       WAGALATIA 1:3    "Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa MUNGU BABA, na kwa BWANA wetu YESU KRISTO, ambaye ALIJITOA nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ILI ATUOKOE na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda MUNGU, BABA YETU" 

      Ubarikiwe sana kwa kufuatana nami katika somo hili. 
UTUKUFU Kwa MUNGU BABA, MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO MTAKATIFU aliyewafunulia WANA WAKE siri za UFALME WA MBINGUNI! 
  
Amen. 
075377548
JEMRATH.





Saturday, 11 March 2017

IJUE KWELI YA MUNGU KUHUSU UFALME WA MUNGU ,KANISA LA MUNGU .


 Ninakusalimu katika jina la BWANA WETU YESU KRISTO ALIYE HAI.

Nakukaribisha katika blog hii ambapo utapata kujifunza mengi kuhusu UFALME WA MUNGU,WOKOVU na mengine mengi ya kimasisha.

SOMO:  KANISA LA MUNGU NA HUDUMA ZAKE( JIFUNZE KUHUSU KANISA)

  

A:KANISA LA BWANA YESU KRISTO.
     I.        Maana ya Kanisa.
   II.        Aina za kanisa .
 III.        Chanzo cha kanisa la Agano jipya.
 IV.        Mifano ya kanisa.
   V.        Kazi (HUDUMA ZA KANISA).
 VI.        Nafasi ya ROHO MTAKATIFU katika Kanisa.                                                                                                                                                              VII.        Hitimisho .

1.    MAANA YA KANISA
Maana isiyo ya Kibiblia.
·         Jengo la kanisa mara nyingi watu huita KANISA.-katika agano la kale majengo haya yalitwa;SINAGOGI,HEKALU.
·         Dhehebu au kundi la watu katika dini ya Kikristo.

  Maana ya “KANISA” katika Agano la kale
v  Neno  KANISA ni asili yake limetokana na nene la kiyunani linaloitwa   EKKLESIA
v   Neno –EK likiwa na maana ya “KUTOKA KWA”
v  Neno – KLESIA lina maana ya “KUITWA”
v  Neno  EKKLESIA” likiwa na maana ya –KUITWA KUTOKA KWA.
v  HIVYO neno
 KANISA katika Agano la kale lilimaanisha ;watu ambao wameitwa kutoka kwenye DHAMBI na dunia na ambao wamekusnyika kwa lengo moja.
Maana ya KANISA katika Agano jipya
ü  Waumini wa kwanza katika Agano jipya, walitumia neno kanisa kumaanisha ifuatvyo;


ü  MKUSANYIKO WA WAAMINI NA WAUMINI katika IMANI YA KRISTO.
ü  WARUMI 16:4-15; NISALIMIENI NA KANISA LILILOMO KATIKA NYUMBA YAO.
ü  WAGALATIA 1:2, 1THESALONIKE 1:1.

ü  Ni kundi lote la watu waliozaliwa mara ya pili( UMOJA WA WAKRISTO ULIMWENGUNI KOTE) 1PETRO 1:23. Yakobo 1:18,
ü  Watu walionunuliwa kwa damu ya YESU KRISTO. MATENDO YAMITUME 20:28. UFUNUO 14:4-5.

2.    AINA ZA KANISA
                                                     I.        JENGO
                                                   II.        WATU WA MAHALI PAMOJA
                                                 III.        MTU BINAFSI(MIMI NA WEWE)

3.    CHANZO CHA KANISA LA AGANO JIPYA.
v  MSINGI WA KANISA hili NI YESU KRISTO , BWANA NA MWOKOZI WETU.
v  Kanisa sio shirika la kibinadamu ,kama wengine walivyolifanya.
v  MATHAYO 16:18, “NA JUU YA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA LANGU;WALA MILANGO YA KUZIMU HAITALISHINDA
v  WAEFESO 2:20-22.
v  KANISA LA KRISTO lilizaliwa SIKU YA PENTEKOSTE,ambayo Ahadi ya BABA ya ROHO MTAKATIFU ,ilitimia na MITUME WAKAJAZWA ROHO MTAKATIFU
v  MATENDO 2:1-4, MATENDO 2:41. Watu elfu tatu walipata wokovu siku hiyo, na KANISA likaanzia hapo.

WASHIRIKA  WA KANISA
a)    Mtu anakuwa mshirika wa KANISA la KRISTO mara tu baada ya KUOKOLEWA (MATENDO 2:27)
b)    Watu wengi wamekuwa washirika wa madhehebu mbalimbali ya dini,,bila kuwa WASHIRIKA WA KANISA LA KRISTO.
c)    MTU anapokuwa MKRISTO anahitaji kuungana NA WAUMINI wa KANISA la BWANA ili KUIMARISHA kanisa LA MUNGU.
d)    WASHIRIKI WA KANISA LA KWELI
ü  NI WATAKATIFU-Tumetenganishwa na maisha ya dhambi na tunamwishia MUNGU. WARUMI 1:7
ü  NI NDUGU. WARUMI 8:29
ü  NI WAAMINI.
ü  NI WATEULE.

4.    MIFANO YA KANISA
                                     I.        KANISA NI BIBI –ARUSI NA MWANAKONDOO
v  UFUNUO 21:2
“Nami nikauona mji ule mtakatifu,Yerusalemu  mpya,ukishuka kutoka mbinguni kwa MUNGU,umewekwa tayari,kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe
v  UFUNUO 21:9, MATHAYO 25:6,, YOHANA 3:29. UFUNUO 19:7.
v  BWANA –ARUSI NI YESU KRISTO, KANISA LINAPASWA KUJENGA MSINGI WAKE katika UTAKATIFU.

                                  II.        MASKANI YA MUNGU (HEKALU LA BABA,MWANA NA ROHO MTAKATIFU)
·         YOHANA 14:23    “YESU akajibu,akamwambia,Mtu akinipenda,atalishika neno langu; na BABA  yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya MAKAO kwake
·         YOHANA 14:16-17    “ Nami nitamwomba BABA, naye atawapa Msaidizi mwingine,ili AKAE nanyi hata milele” “bali ninyi mnamtambua ,maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu”
·         1WAKORINTO 6:19-20    AU hamjui ya kuwa mwili wenu ni HEKALU LA ROHO MTAKATIFU aliye ndani yenu,mliyepewa na MUNGU? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; Maana  mlinunuliwa kwa THAMANI. Sasa basi,mtukuzeni MUNGU katika miili yenu.
·         UFUNUO 21:3, 1KORINTO 3:16, 2KORINTO 6:16.
·         KILA mshirika wa KANISA la KRISTO ATAMBUE uthamani huu MKUU tuliopewa na MUNGU,,ili TUWEZE KUKAA katika hali YA UTAKATIFU.

                                III.        MWILI WA KRISTO YESU,MWOKOZI.
Ø  1WAKORINTO 12:24-37.  27  BASI NINYI MMEKUWA MWILI WA KRISTO,NA VIUNGO KILA KIMOJA PEKE YAKE”
Ø  YESU NDIYE BWANA na KIONGOZI MKUU wa kanisa.
Ø  KILA MUUMINI,ni mshirika wa MWILI HUU.
Ø  Wauumini wanahitaji kushirikiana ili waweze kuishi katika MWILI wa KRISTO.
Ø  KILA mwamini ni Mtu na kiungo MUHIMU cha KANISA. Hata kama kinadharauliwa na kuonekana ni cha kawiada bado NI CHA MUHIMU SANA.
Ø  KILA mshirika katika MWILI huu lazima awe na uhusiano wa moja kwa moja na MKUU WA KANISA –YESU KRISTO.
Ø  KANISA NI MWILI WA KIROHO WA YESU kujidhihirisha kwa ULIMWENGU.
Ø  Hivyo washirika,  wote  tunapaswa kuhimizana,kusaidiana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuujenga mwili wa KRISTO.
Ø  WAEFESO 4:16  Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila KIUNGO,kwa kadri ya utendaji wa kila sehemu moja kwa moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika UPENDO

                                 IV.        KANISA NI NGUZO NA MSINGI WA KWELI
1TIMOTHEO 3:15
NI mahali ambapo watu hufundishwa kweli yote ya NENO LA MUNGU.

                                   V.        KANISA NI CHOMBO MILIKIWA NA MUNGU MWENYEWE
TITO 2:14. ,  1 PETRO 2:9
ü  NYUMBA YA ROHO
ü  UKUHANI MTAKATIFU
ü  MAWE YALIYO HAI
ü  MZAO MTEULE
ü  UKUHANI WA KIFALME
ü  TAIFA TAKATIFU
ü  WATU WA MILIKI YA MUNGU.
ü  TAIFA LA MUNGU.

5.    KAZI (HUDUMA YA KANISA LA KRSTO)
MUNGU ,BWANA YESU KRISTO aliweka na kuanzisha KANISA ili kuleta UTUKUFU WA JINA LAKE.
v  Kazi hizi tunaweza kuziangalia katika sehmu tatu ambazo zinamtukuza MUNGU
                                                     i.        KWA NJE’ > INJILI YA YESU KRISTO
                                                    ii.        KWA NDANI’ > TUNAPOJENGANA SISI KWA SISI
                                                  iii.        ‘KWA JUU’ >KATIKA IBADA


KAZI ZA KANISA
A.     Kuhubiri injili kwa  kila kiumbe ulimwenguni kote( HABARI NJEMA ZA UFALME WAMUNGU)
MARKO 16:15, MATHAYO 28:19-20.   1PETRO 2:9,MATENDO 1:8.
B.   Kujengana Nafsi (mwili wa KRISTO)  1KORINTO 14:26.
C.   HUMFANYIA MUNGU IBADA . WEABRANIA 13:15, 10:25.  NJIA ambazo tunamwabudu MUNGU
v  Kukusanyika pamoja, mathayo 18:20,,ebrania 10:25.
v  Kupitia mziki na nyimbo. Waefeso 5:19,, zaburi 50:23,ZABURI 150
v  Kwa njia ya MAOMBI        .MATENDO 2:46-47,4:24. MARKO 11:17
v  KUTOA
v  Kwa NJIA YA ROHO MTAKATIFU
v  KUHIDHABIHU NMIILI YETU, WARUMI 12:1-2.
D.KANISA HUMRUSU ROHO MTAKATIFU katika HUDUMA ZOTE. 1KORINTO 12:4
E.HUFUNDISHA KWELI YA NENO LA MUNGU.kupitia vipindi mbalimbali,Sunday school,vijana.
F.HUBATIZA KWA MAJI MENGI. MATHAYO 28:19
G.HUKUMBUKA KIFO CHA BWANA kwa njia ya MEZA YA BWANA. LUKA 22:20.
H. HUFANYA USHIRIKA MBALIMBALI, kuomba kwa pamoja, kula kwa pamoja na kushirikiana.
I.kanisa HUSHEREKEA, mfano;ndoa,watoto kuombewa,vifo, Christmas,pasaka,siku  ya BWANA
J.KANISA HUKUA
K.HUHUDUMIA WATU; KUSAIDIA wahitaji,waliopotea,na kuwalea waumini wapya.
PIA kazi nyingine muhimu ni pamoja na
v  KUMTII KRISTO kwa kuwatii wnadamu. WAEBRANIA 13:17, TITO 3:1-2. 1THESALONIKE 5:12, MALAKI 2:7.
v  KUITEGEMEZA NYUMBA YA MUNGU
v  KUIJENGA NYUMBA YA KUABUDIA
v  KUITEGEMEZA NYUMBA YA MCHUNGAJI
v  1WAKORINTO 9:7-11; MATHAYO 25;31-46;
v  KUTOA ZAKA   MALAKI 3:10-12., MITHALI 10:27. MITHALI 3:9-10.


6.    NAFASI YA ROHO MTAKATIFU KATIKA KANISA LA LEO. ROHO wa MUNGU ndio chanzo cha KANISA LA KWANZA ,hivyo basi tunapaswa kutambua na kumpa nafasi ya PEKEE na ya  KWANZA katika MAISHA YETU na HUDUMA katiKA kanisa lake.
ü  Wagalatia 4:6, waefeso 4:4
ü  YEYE ndiye kiongozi,mwalimu wetu  hivyo ni vyema katika maamuzi yote tuyafanyayo KUMSHRIKISHA ili tuweze kukua KATIKA IMANI YA YESU KRISTO.
ü  KANISA ,tunapaswa kusisitiza kila mmoja wetu, kuhusu KUJAZWA NA kutembea,kuishi katika ROHO MTAKATIFU

7.    HITIMISHO
“KANISA ni MWILI HALISI WA KIROHO WA YESU KRISTO, hivyo tunapaswa kuwa na kutmbea na kuishi katika UTAKATIFU
v  LUKA 18: 7-8  NA MUNGU,JE! HATAWAPATIA HAKI WATEULE WAKE WANAOMLILIA MCHANA NA USIKU, NAYE NI MVUMILIVU KWAO?8 NAWAAMBIA,ATAWAPATIA HAKI UPESI; WALAKINI, ATAKAPOKUJA MWANA WA ADAMU, JE!ATAIONA IMANI DUNIANI?
HESHIMA NA UTUKUFU KWAKO BWANA NA MWOKOZI WETU YESU KRISTO UNAYE TUWEZESHA! Barikiwa sana wote.By jbrev.







     

Thursday, 9 March 2017

MAOMBI YA KUPATA MAJIBU TOKA KWA MUNGU

   Rafiki, ndugu na mpendwa ninawasalimu wote katika JINA LAKE YESU KRISTO ALIYE HAI MILELE. 
   karibuni sana katika blog hii itakayokupa masomo kuhusu UFALME WA MUNGU, WOKOVU na  mengine ya kimaisha! 

SOMO 1:MAOMBI 
MAOMBI/KUOMBA NI kitendo cha kuwa na USHIRIKA na Mungu WAKO kila siku katika maisha yako, inahusisha KUPELEKA mahitaji yako KWAKE, kumwabudu na kumsifu n. K YAKOBO 5:17, IWAFALME 18 :41-46.

(a) MAMBO YA MSINGI KATIKA MAOMBI 
 1.Kuomba kwa BIDII  
2.Kuomba kwa UHAKIKA 
3.Kupata majibu 
4.Kuyafanyia KAZI (MAOMBI kwenye Matendo) MARKO 2:11 

(b) VITU VINAVYOONDOA UHAKIKA NDANI YAKO UKIWA UNAOMBA. 
1.Dhambi 
2.Elimu 
3.Msululu wa shida zisizoisha 
4.Mafundisho ya Uongo. 

(c) MAADUI WA MAOMBI 
1.UVIVU, Yakobo 5:16-17 
2.MASHAKA, Yakobo 1:6-7 
3.DHAMBI, Yohana 9:31, Isaya 1:15 
4.KUTOKUSAMEHE, MARKO 11:25-26 

(d) MAMBO YANAYOJENGA UHAKIKA KATIKA MAOMBI 
1 NENO LA MUNGU 
2.YESU KRISTO NA ROHO MTAKATIFU 
3.UUMBAJI WA MUNGU.
4.DHAMIRI ZETU.
   
KUMBUKA YAFUATAYO KWA LEO. 
1.Maombi yana nguvu zaidi ya upako na nguvu ulizonazo katika Huduma (PRAYER IS MORE POWERFUL THAN POWER) 
2.Shetani anaogopa sana MTU wa  Maombi, haogopi upako, Huduma, elimu, fedha, umaarufu. KITU kinachomtisha NI MAOMBI KWA MUNGU BABA! 
3.Maombi yafanyike sehemu ya Maisha yako, sio kwa kujisikia, hata kama hausikia msukumo wa KUOMBA, we OMBA! 
4.UANAPOOMBA KWA MUNGU KUWA MWAMINIFU katika IMANI na KUTUNZA KILE ULICHOOMBA hata kama hakitajibiwa kwa wakati huo. 
5.Maombi yako yasipojibiwa, USIPOTEZE IMANI Kwani UNAPOAMUA KUOMBA KWA MUNGU, uwe tayari Kupokea Majibu au La, MUNGU hujibu kwa Wakati sahihi! 

          "ASANTENI SANA, tunaendelea kujifunza somo hili kwa undani ZAIDI, hiyo ni mwanzo, karibuni sana wote, BWANA YESU KRISTO AWABARKI SANA, ANAWAPENDA WOTE!