Thursday, 9 March 2017

MAOMBI YA KUPATA MAJIBU TOKA KWA MUNGU

   Rafiki, ndugu na mpendwa ninawasalimu wote katika JINA LAKE YESU KRISTO ALIYE HAI MILELE. 
   karibuni sana katika blog hii itakayokupa masomo kuhusu UFALME WA MUNGU, WOKOVU na  mengine ya kimaisha! 

SOMO 1:MAOMBI 
MAOMBI/KUOMBA NI kitendo cha kuwa na USHIRIKA na Mungu WAKO kila siku katika maisha yako, inahusisha KUPELEKA mahitaji yako KWAKE, kumwabudu na kumsifu n. K YAKOBO 5:17, IWAFALME 18 :41-46.

(a) MAMBO YA MSINGI KATIKA MAOMBI 
 1.Kuomba kwa BIDII  
2.Kuomba kwa UHAKIKA 
3.Kupata majibu 
4.Kuyafanyia KAZI (MAOMBI kwenye Matendo) MARKO 2:11 

(b) VITU VINAVYOONDOA UHAKIKA NDANI YAKO UKIWA UNAOMBA. 
1.Dhambi 
2.Elimu 
3.Msululu wa shida zisizoisha 
4.Mafundisho ya Uongo. 

(c) MAADUI WA MAOMBI 
1.UVIVU, Yakobo 5:16-17 
2.MASHAKA, Yakobo 1:6-7 
3.DHAMBI, Yohana 9:31, Isaya 1:15 
4.KUTOKUSAMEHE, MARKO 11:25-26 

(d) MAMBO YANAYOJENGA UHAKIKA KATIKA MAOMBI 
1 NENO LA MUNGU 
2.YESU KRISTO NA ROHO MTAKATIFU 
3.UUMBAJI WA MUNGU.
4.DHAMIRI ZETU.
   
KUMBUKA YAFUATAYO KWA LEO. 
1.Maombi yana nguvu zaidi ya upako na nguvu ulizonazo katika Huduma (PRAYER IS MORE POWERFUL THAN POWER) 
2.Shetani anaogopa sana MTU wa  Maombi, haogopi upako, Huduma, elimu, fedha, umaarufu. KITU kinachomtisha NI MAOMBI KWA MUNGU BABA! 
3.Maombi yafanyike sehemu ya Maisha yako, sio kwa kujisikia, hata kama hausikia msukumo wa KUOMBA, we OMBA! 
4.UANAPOOMBA KWA MUNGU KUWA MWAMINIFU katika IMANI na KUTUNZA KILE ULICHOOMBA hata kama hakitajibiwa kwa wakati huo. 
5.Maombi yako yasipojibiwa, USIPOTEZE IMANI Kwani UNAPOAMUA KUOMBA KWA MUNGU, uwe tayari Kupokea Majibu au La, MUNGU hujibu kwa Wakati sahihi! 

          "ASANTENI SANA, tunaendelea kujifunza somo hili kwa undani ZAIDI, hiyo ni mwanzo, karibuni sana wote, BWANA YESU KRISTO AWABARKI SANA, ANAWAPENDA WOTE!  



1 comment: