Monday, 24 July 2017

UWAKILI WA MUNGU (STERWARDSHIP OF GOD)


  • Hellow watu wa MUNGU, nakukaribisha katika blog hii ambayo unapata masomo mbalimbali kuhusu UFALME WA MUNGU na Maisha yako. Ubarikiwe sana. Karibuni sana.


SOMO :UWAKILI WA MUNGU.  SISI NA VITU VYOTE NI MALI YA BWANA.

Mwanzo 1:1 " HAPO MWANZO MUNGU ALIZIUMBA MBINGU NA NCHI"   MUNGU ndiye mmiliki wa kila kitu, aliyeumba, NDIYE ANAYEMILIKI VITU VYOTE!
ZABURI 24 :1 "NCHI NA VYOTE VIIJAZAVYO NI MALI YA BWANA, DUNIA NA WOTE WAKAAO NDANI YAKE" 


A. MAANA YA WAKILI : Ni mtu aliyepewa dhamana juu ya mali ya mtu mwingine! 

KUMBUKA, katika kitabu cha MWANZO 1:28-31. Mungu MUUMBA alitukabidhi mali yake ili tuitunze kwa UTUKUFU wake.
WAKILI (manager, steward, administrator).


  • UWAKILI unaonyesha mahusiaano makubwa kati ya Mungu na Mwanadamu.  "GOD as a OWNER and Man as a MANAGER"

MUNGU ametuweka sisi kuvisimamia vitu vyote tulivyo navyo katika maisha yetu. (it is a DIVINE TRUST).

SIFA KUU ZA MAWAKILI AMBAO MUNGU ANATAFUTA. 
1.MAWAKILI WAAMINIFU.
2.MAWAKILI WENYE BUSARA.

  • WAKILI MWAMINIFU ni yule anayetambua kwamba yeye na vitu alivyonavyo ni MALI YA MUNGU. Pia huishi na kutumia vyote kwa ajili ya MUNGU. 

  • WAKILI Mwenye BUSARA huilinda mali ya BWANA wake na kuendelea kuzalisha na kuzaa matunda mpaka BWANA wake ATAKAPOKUJA, hakati tamaa, NI mvumilivu. Anawajibika kwa mali ya BWANA wake. (LUKA 12:42-48). 

MATHAYO 25 :14 - 30. (WATUMISHI waliopewa TALANTA).


  1. HAGAI 2:8 "Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, ASEMA BWANA wa MAJESHI. 
  2. ACTS 17 :25" Kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na Pumzi yangu, ASEMA BWANA "
SISI sio wamiliki wa maisha yetu na vitu vyetu, MUNGU ametuweka kuwa MAWAKILI WAKE. 1WAKORINTO 4:1-2" Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa KRISTO na MAWAKILI wa siri za MUNGU. Hapo tena inayohitajiwa katika MAWAKILI, ndiyo Mtu aonekane kuwa MWAMINIFU "

N.B :WAKILI MWEMA anafanya mambo yote kwa faida na HESHIMA na UTUKUFU WA BWANA WAKE.

B:MAENEO YETU YA UWAKILI, AMBAYO MUNGU AMETUPA!

  1. UWAKILI WA MUDA WETU. Muda ni  kitu cha muhimu Sana, kwa sababu muda ukipita umepita, haujirudii tena. Tunapaswa kutumia mda wetu vizuri kwa UTUKUFU wa MUNGU.                                                                                                                                  Pia tunahitaji kutumia muda wetu vizuri kwa ajili ya HUDUMA, KAZI, FAMILIA., Masomo.  1PETRO 4:2.    , 1 korinto 10:31.                                                                Waefeso 5:15-16 "MKIUKOMBOA WAKATI KWA MAANA ZAMANI HIZI NI ZA UOVU".
Tusitumie mda huu mchache tuliopewa na MUNGU duniani kufanya yasiyo mpendeza, bali TAFUTA KUYAFANYA MAPENZI YA MUNGU kila mda, Pangilia mda wako na TUMIA MDA HUU KUYAANDAA MAISHA YAKO YA MILELE. Baada Ya mda huu hatutapata mda . Mwingine. 
     2. UWAKILI WA MIILI YETU. 

  • Tumeumbwa kwa sura na mfano wa MUNGU. 
  • Mungu anaagiza tuitoe miili yetu iwe dhabihu na kuifanya ibada. 
  • Tunapaswa kumpenda MUNGU kupitia miili yetu.  WARUMI 12:1. 
  • Miili yetu ni mahekalu ya ROHO MTAKATIFU. 1 korinto 3:16 " au hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hakalu la ROHO MTAKATIFU na ya kuwa Roho wa anakaa ndani yenu?. 
  • Kuishi maisha matakatifu na kujitenga na dunia na kumkaribia MUNGU. 
  • Hatupaswi kuitumia miili yetu kwa dhambi na uovu.   
  • Pia MUNGU anatamani tuitunze miili yetu na afya zetu,, kula vizuri, PUMZIKA, fanya mazoezi. 
  • Tuishi kwa ajili ya MUNGU tu 1.Kumuabudu 2.Kumtii 3.Kuwa HAI katika Bwana na kufa kwa habari ya dhambi. 
          3.UWAKILI WA MALI ZETU. 
"KUTOKA 19 :5 "Maana dunia yote ni mali yangu"   Tukumbuke kwamba ndiye  anaayetupa mali na vitu vyote tulivyo navyo. Tunapaswa kuvitumia kueneza UFALME WAKE

AYUBU 41 :11 "Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe? Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni CHANGU" 
MUNGU anaagiza tutumie mali tulizopewa kwa ajili ya UTUKUFU wake, mfano, Nyumba, gari, Ardhi. 

         4.UWAKILI WA KARAMA, VIPAWA, TAALUMA NA HUDUMA
MFANO, Uimbaji, karama za ROHONI, Udaktari, Ualimu, komputya, ufundi umeme, na kila Kazi yoyote unayofanya. 
Vyote hivyo, MUNGU amekupa kwa ajili ya kutumika Kuujenga UFALME WAKE UNAVITAWALA.. WAEFESO 4:11 - 16. 

5.UWAKILI WA FEDHA ZETU NA UTAJIRI
Mungu ametupa fedha kwa ajili ya UTUKUFU wake na kueneza Kazi yake. KURUDI la Mungu kuhusu Fedha ni kuwabariki Watoto wake, kutuwezesha Kuishi maisha yenye BARAKA KWA kujifunza KUTOA NA KUPOKEA!

KWA NINI TUTOE FEDHA ZETU.

  1. BIBLIA TAKATIFU INATUFUNDISHA UTOAJI (malaki 3:8-12) 
  2. NI AGIZO LA YESU (LUKA 6:8) 
  3. TUNAONYESHA UPENDO WETU KWA MUNGU (1 korinto 13 :4)
  4. TUNAWEKA HAZINA KWA MUNGU. 
  5. NI HERI KUTOA KULIKO KUPOKEA Acts 20:35). 
  6. KRISTO mwenyewe ALIJITOA kama sadaka kwa ajili yetu. 
  7. KWA AJILI YA KUENEZA UFALME WA MUNGU NA KAZI YA MUNGU DUNIANI. 
  8. Tunapaswa kumtolea MUNGU kwa HIARI, FURAHA, UTIIFU, UHURU, UWIANO, UKARIMU NA KWA DHABIHU. 
  9. Tukumbuke kumtolea MUNGU ZAKA (FUNGU LA KUMI) MWANZO 14 :18-20) SADAKA inayonyesha kwamba MUNGU NDIYE ANAYEMILIKI. 
    C: FOUR PRINCIPLES OF STEWARDSHIP!

THE FUNDAMENTAL PRINCIPLE OF ALL PEOPLE States that " we own nothing, God owns everything, we are simply managers "

1.THE PRINCIPLE OF OWNERSHIP (UMILIKI) Genesis 1:1,ZABURI 24. God created everything, He only owns everything.

2.THE PRINCIPLE OF RESPONSIBILITY (UWAJIBIKAJI). Mungu ana HAKI ya UMILIKI, MAWAKILI wana wajibika. Mungu ametuita kusimamia MALI yake,Tunapaswa kuwajibika.

3.THE PRINCIPLE OF ACCOUNTABILITY. (KUTOA HESABU)   WARUMI 14 :12 "Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za MUNGU"
Tutatoa HESABU ya vile tilivyokabidhiwa (Time, money, ability, information, wisdom, authority, talents, work Education, relationship, resources and opportunities).

4.THE PRINCIPLE OF REWARD ( MALIPO).  
MATHAYO 25 :21 "BWANA wake akamwambia, vema, mtumwa mwema na MWAMINIFU, ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya Mengi, ingia katika FURAHA YA BWANA wako"
Wakolosai 3:23 - 24.

MUHIMU SANA :"There is no greater choice offered to us than surrender to the one who CREATED us and knows us better than we know ourselves "

SWALI LA KUKUMBUKA :LUKA 18 :8  " WALAKINI, ATAKAPOKUJA MWANA WA ADAMU, JE, ATAIONA IMANI DUNIANI?

ubarikiwe sana kwa kujifunza. UTUKUFU KWA MWOKOZI YESU KRISTO ANAYEOKOA NA KUTUPA ROHO MTAKATIFU KUTOKA KWA MUNGU BABA. Amen.

Jemrath Bikombo.

16 comments:

  1. Mungu akubariki sana MTU wa Mungu endelea kufanya hivi maana tunabarikiwa sana

    ReplyDelete
  2. Mungu akubariki sana MTU wa Mungu endelea kufanya hivi maana tunabarikiwa sana

    ReplyDelete
  3. Be blessed for this important semon of stewardship you gave us, it will be remembered even in the holly day of coming to Jesus.

    ReplyDelete
  4. Nitumie hapo sifa kuu za wakili mwaminifu

    ReplyDelete
  5. Ubarikiwe sana mtumishi kwa neno zuri

    ReplyDelete
  6. Ubarikiwe sana Mtumishi kwa somo Zuri

    ReplyDelete
  7. Umenibariki mtumishi. Kuna kitu nimejifunza kitanisaidia sana

    ReplyDelete
  8. Mungu hakubariki mtumishi Wa Mungu

    ReplyDelete
  9. Sifa za wakili mwaminifu na hasara za kutokuwa wakili mwaminifu

    ReplyDelete
  10. Iko vema sana,matumizi mazuri ya kimtandao tunapata vitu vizur sana Mungu atupe namna ya kuyaishi maandiko

    ReplyDelete